TEKNOLOJIA MPYA YA WEHOLITE KUSAIDIA UDHIBITI WA MAFURIKO NA MAJI TAKA
KAMPUNI ya Plasco Limited ambayo ni watengenezaji wa bidhaa za mabomba makubwa ya plastiki yatumikayo kwenye ujenzi wa miundombinu, imeleta Teknolojia mpya ya utengenezaji mabomba hayo iitwayo Weholite itakayosaidia kutoa suluhisho za changamoto za miundombinu ya zamani na kuboresha udhibiti wa maji taka na kuhifadhi mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya wanahabari katika kiwanda cha mabomba cha Plasco kilichopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Muendeshaji wa kiwanda hicho, Alimiya Osman amesema kampuni hiyo inajivunia kutumia teknolojia ya Weholite, kutoa suluhisho kwa miradi ya ujenzi haswa katika maji taka na udhibiti wa mafuriko
Amesema, utimiwaji wa Teknolojia ya Weholite utasaidia pia kurahisihwa kwa kazi hasa wakati wa kurekebisha miundonbinu ya barabara kwa kuifanya kutofungwa kwa muda mrefu na hivyo wakati mwingine kusababisha foleni na kuathiri uchumi wa nchi kutokana na watumiaji wa eneo la barabara kulazimika kuchukua muda mrefu barabarani wakisubiri eneo husika kurekebishwa
Amesema, Weholite ikitumika kwa ajili ya karavati za barabarani badala ya zile karavati za zege, itaokoa muda kwani miundombinu ya barabara haitafungwa kwa muda mrefu labda siku mbili wakati ya zege hutumia hata mwezi kukamilika na kuwafanya watumiaji wa barabara husika kutumia muda mwingi njiani sababu barabarani.
"Mfano Dar es Salaam leo ikinyesha mvua inakuwa ni tatizo sana, miundombinu ya maji taka inafurika sababu ya ongezeko la watu huku miundombinu yetu ikibakia kuwa ni ya kizamani na hivyo kunanahitajika maboresho ili kukidhi mahitaji yetu..., tunahamasishana tuangalie uwezekano wa kutumia teknolojia hii katika miradi yetu mbali mbali ya miundombinu kwa Maendeleo ya nchi yetu.'' Amesema Osman.
Aidha amesema Weholite pia inatumika kwa kutengeneza matanki makubwa ya kuhifadhi maji safi ambapo kwa kutumia Weholite tanki linaweza kudumu kwa vizazi, kawaida hadi miaka mia moja ikilinganishwa na saruji ambayo inaweza kudumu kwa miaka 20 tu lakini pia Weholeti ina sifa kadhaa ambazo hufanya suluhisho bora na bora, kwa mfano ina maji ya kujitakasa na mgawo mdogo wa msuguano, inahitaji utunzaji mdogo, ni rahisi na haraka kufunga na gharama nafuu.
Mbali na mafanikio hayo, Osman amesema walikuwa wakipata changamoto ya soko kwa kulazimika kuuza bidhaa zao kwa garama za chini ili kushindana na bidhaa zinazotoka nje ya nchi kitendo ambacho kilikuwa kukiwakosesha faida lakini sasa Serikali imeweza kudhibiti bidhaa hizo kuingia nchini na hivyo viwanda vyetu sasa vimepewa nafasi ya kufanya kazi.
No comments: