TCRA YATOA MSAADA KWA VITUO VITATU VYA KULELEA WATOTO YATIMA MKOANI PWANI
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jumanne Ikuja akimkabidhi Msaada wa Vitu mbalimbali Mkuu wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Salom Lilian Mbise wakati Mamlaka hiyo ilipokwenda kutoa msaada katika hicho kilichopo Kwamathias Kibaha mkoani Pwani.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jumanne Ikuja akimkabidhi Msaada wa Vitu mbalimbali Mratibu wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Fadhila Shokat Ibrahim wakati Mamlaka hiyo ilipokwenda kutoa msaada katika hicho kilichopo Misugusugu Kibaha mkoani Pwani.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jumanne Ikuja akimkabidhi Msaada wa Vitu mbalimbali Mkuu wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Salom Lilian Mbise wakati Mamlaka hiyo ilipokwenda kutoa msaada katika hicho kilichopo Kwamathias Kibaha mkoani Pwani.
Wanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Fadhila mara baada ya kutoa msaada katika kituo hicho kilichopo Msugusugu. wilayani Kibaha mkoani Pwani
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Mwandamizi wa Mamlaka hiyo Jumanne Ikuja akizungumza na watoto na watendaji wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Salom kilichopo Kwamathias wilayani Kibaha mkoani Pwani mara baada ya kukabidhi msaada katika kituo hicho.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Amani kilichopo Zinga wilayani Bagamoyo Margareth Mwegalava akizungumza kuhusiana na historia ya kituo hicho wakati TCRA ilipokwenda kutoa msaada.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jumanne Ikuja akimkabidhi Msaada wa Vitu mbalimbali Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Amani Margareth Mwegalava wakati Mamlaka hiyo ilipokwenda kutoa msaada katika hicho kilichopo Zinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Wafanyakazi wa TCRA Kanda ya Mashariki wakiwa wameshika watoto yatima katika kituo cha kulelea watoto Yatima kilichopo Zinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Wafanyakazi wa TCRA Kanda ya Mashariki wakifurahi na watoto yatima wa kituo cha kulelea watoto hao kilichopo Kwamathias wilayani Kibaha mkoani Pwani.
*Waahidi kuendela kusaidia kwa kuwa ni sehemu ya jamii
*Wenye vituo watoa ya moyoni baada ya kupata msaada
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imetoa msaada wa vitu mbalimba kwenye vituo vitatu vya kulelea yatima mkoani Pwani.
Vituo vitatu vimepata msaada kutokana na mahitaji yao ikiwemo kukidhi kusherekea sikukuu za Krismasi na mwaka mpya pamoja na kuwasaidia katika kipindi kifupi baada ya kumalizika sikukuu ambavyo ni Shalom kilichopo Kibaha kwa Mathias, Fadhila Kilichopo Misugusugu pamoja na Amani kilichopo Zinga Bagamoyo.
Mahitaji ya vituo hivyo vimepata mbuzi mbili kwa kila Kituo , Mchele, Maharage, Mafuta ya Kupikia, Sabuni za Unga, Sabuni za vipande, Maziwa ya Kopo, katoni za Shurubati, Katoni za Soda, Katoni za Chumvi, Dawa za mswaki, Mafuta ya Kupaka, na Taulo kwa ajili ya Watoto wa Kike.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika vituo vya Kulelea Watoto Kwa niaba ya Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA, Mhandisi Mwandamizi Jumanne Ikuja amesema kuwa Mamlaka kwa kutambua uhitaji wa jamii, imetoa vitu hivyo ili viweze kuwasaidia watoto kusherekea sikukuu za msimu huu na pia kuendelea kuwasaidia kwa siku chache baada ya sikukuu.
Amesema kuwa msaada huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba katika utaratibu wa Mamlaka wa kutekeleza majukumu ya taasisi kwa jamii. Huu ni utaratibu wa TCRA katika kuungana na jamii hiyo kwa kutambua hawana watu maalum wa kusaidia bali ni jamii nzima inawajibika kuwasaidia watoto hao.
Ikuja amesema kuwa watu wanaosimamia vituo hivyo wamejitoa katika kuhakikisha jamii yote inakuwa sawa katika kulea Watoto ili kuweza kukua na kufikia malengo yao kwa kufanya wawe watu wazima wa kujisimamia wenyewe.
"Kama Kanda tumejitahidi na kuweza kupata kile ambacho tumeweza kujaliwa kwa kushiriki pamoja na watoto wetu hawa wasijisikie hawako pekee yao na hivyo leo tunakabidhi vyakula na vifaa hivi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA." amesema Mhandisi Ikuja.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto cha Amani Ndugu Margareth Mwegalava amesema wakati kituo kinakabiliwa na changamoto za kuendesha masuala mengine ikiwemo bili ya Maji na changamoto ya Umeme wa Jua (Solar.)
Amesema kuwa msaada huo kwao ni mkubwa sana utaweza kumsukuma kwa kipindi kifupi. Ameeleza kuwa Watoto wengi katika Maeneo ya Bagamoyo wanaowapata wanakuwa wametupwa na wengine wanakuwa wametoka Mikoa mingine.
Mkuu wa Kituo cha Shalom Lilian Mbise amesema kuwa msaada huo umekuja kutoka kwa Mungu kwa kuonyesha TCRA kupeleka msaada kwani chakula alikuwa ameishiwa huku akiwa na changamoto ya kuongeza vitanda na kuboresha jengo ambalo ndio la kituo kwani awali walikuwa wapangaji.
Kwa upande wa Mratibu wa Kituo cha Kulelea Watoto cha Fadhila kilichopo Misugusugu, Kibaha Shokat Ibrahim amesema kuwa wanaishukuru TCRA kwa kutambua kwa kuwaona wao kwani vituo ni vingi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia jamii hiyo.
No comments: