SPIKA NDUGAI ATAKA MAJENGO YOTE YA UMMA MAPYA KUWAJALI WATU WENYE ULEMAVU
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Watu Wenyeulemavu kitaifa zilizofanyika Wilaya ya Kongwa jijini Dodoma. |
|
Baadhi ya wageni, wadau na watu wenye ulemavu wakipata machapisho yenye jumbe mbali kwenye banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET). |
Baadhi ya wageni, wadau na watu wenye ulemavu wakipata machapisho yenye jumbe mbali kwenye banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) ndani ya maadhimisho hayo. |
BUNGE la Tanzania litaendelea kupigania uwepo wa miundombinu rahisi na wezeshi ya watu wenye ulemavu kwenye majengo ya umma pamoja na changamoto nyingine kwa kundi hilo maalumu la watu wenye ulemavu, ili kuhakikisha wanapata haki na fursa sawa kama ilivyo kwa watu wengine.
Kauli hiyo imetolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Mh. Job Ndugai alipokuwa akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Watu Wenyeulemavu zilizofanyika, Wilaya ya Kongwa jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wanaofanya kazi na kundi hilo maalum.
Mh. Ndugai amesema Bunge litaendelea kuhimiza majengo yote ya umma yanayojengwa sasa kuzingatia yanakuwa na miundombinu rafiki kuwawezesha kundi la watu wenye ulemavu wanapata huduma katika majengo hayo bila kikwazo chochote.
"...Waheshimiwa madiwani wa Kongwa mpo na madiwani wengine nchi nzima iwe ni madarasa ya shule, iwe ni ofisi za vyama vya siasa, iwe kwa majengo ya Serikali na majengo yoyote yanaotoa huduma za watu wengi, yajengwe kwa taratibu ambazo ni rafiki kwa watu wenyeulemavu, hata nyumba yako mwenyewe unayoijenga jenga kwa taratibu ambayo inaurafiki kwa watu wenye ulemavu...mimi sijui kama kuna familia au ukoo auna watu wenyeulemavu ndani yao. Hii ni kwasababu ni sehemu ya uumbaji wa Mungu na wakati mwingine mtu unaweza kupata ajali yoyote na ukajikuta umekua katika kuni hilo," alisisitiza Mh. Ndugai.
Spika Ndugai pia alishauri taifa kuanza kujipanga namna bora ya kuyawezesha kiuhalisia makundi ya watu wenye ulemavu kwa kutumia fedha zake, pasipo kutegemea wahisani pekee na wadau wengine. Alisema kwa kuwa Bunge limekuwa likipitia bajeti mbalimbali litaendelea kuikumbusha Serikali kuhakikisha suala hilo linapewa kipaombele kadri inavyowezekana.
Aliongeza kuwa Bunge litaendelea kuishauri Serikali kuangalia namna ya ama kuondoa kodi au kupunguza kodi kwa vifaa saidizi vya kundi la watuwenye ulemavu vinavyoingia au kutengenezwa nchini ili viweze kupatikana kwa bei ya chini na kuwasaidia wanaohitaji vifaa hivyo kuwawezesha katika shughuli zao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akielezea namna jeshi hilo linavyowajali watu wa makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu. |
Aidha alisema Bunge katika kipindi cha miaka mitano litahakikisha linaishauri na kuisimamia Serikali ili ile mikopo ya asilimia mbili ya kundi la watu wenye ulemavu ipatikane kwa wahusika huku ikiwa na masharti nafuu, kwani habari ya kusema walemavu wajiunge katika vikundi imekuwa vikwazo kwa baadhi yao, hivyo kuna haja ya kuangalia upya utaratibu huo. "...Wakati mwingine habari za vikundi zinawalazimisha watu hawa kukaa kwenye makundi hata na watu ambao hawana sifa za kuwa kwenye kundi hilo," alisema Spika Ndugai.
Kwa upande wao wadau, ukiwemo Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), wameiomba Serikali kupitia kwa mgeni rasmi Ndugai alipotembelea mabanda ya wadau kwenye maadhimisho hayo, kuhakikisha Baraza la Mitihani (NECTA), linaweka mfumo stahiki wa kuwataini wanafunzi wenye ulemavu unaopima uwezo wao wa kitaaluma kulingana na mahitaji yao.
"...Serikali kushirikiana na wadau wa maendeleo waendelee kutoa vifaa vya kujifunza na kujifunzia mashuleni ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata haki yake ya msingi ya elimu. Serikali pia kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, waendelee kuwajengea uwezo walimu namna ya kuwabaini na kuwafundisha watoto wenye ulemavu kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vikuu," alisema Ofisa Utetezi wa TENMET, Nasra Kibukila akitoa mjumbe wa Serikali kwa Mh. Ndugai alipotembelea banda la mtandao huo.
Alisema Mtandao wa Elimu Tanzania kupitia wanachama wake utaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha elimu itolewayo kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne ipo kwenye viwango bora na inamjengea mtoto uwezo wa kupambana kimaisha. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ambayo ni ya 18 kufanyika tanzania ni; Si kila ulemavu unaonekana.
Mtafsiri wa luga za alama akifikisha ujumbe kwa washiriki anuai kwenye hafla ya Maadhimisho hayo yaliofanyika Kongwa. |
Baadhi ya wageni, wadau na watu wenye ulemavu wakipata wakifuatilia matukio anuai kwenye maadhimisho hayo. |
No comments: