SERIKALI YAWAASA WATAFITI,WABUNIFU NA WAGUNDUZI SEKTA MBALIMBALI KUTUMIA TEKNOLOJIA ZINAZOIBUKA ILI KULETA MAENDELEO NCHINI

 SERIKALI imewaasa watafiti, wabunifu na wagunduzi wa sekta mbali mbali nchini kuchukua hatua za makusudi katika kutumia Teknolojia zinazoibukia ili kuleta Maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Pia ni vema wadau mbali mbali wakatafakari na kujiuliza ni namna gani wanajitayarisha ili kunufaika kikamilifu na mabadiliko ya kiteknolojia na namna mabadiliko hayo yataathiri maisha ya watu wa Vijiji, miji na majiji.

Naibu Katibu Mkuu, wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe ameyasema hayo leo Desemba 4,2020 wakati akifunga mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo washiriki wa Makisatu 2020 juu ya kuendelea bunifu zao na kuwakabidhi mfano wa hundi  wawakilishi wabunifu wa washiriki wa mafunzo

Amesema, mafunzo hayo yamewajengea  uwezo na kuwapa mwanga wa kutambua fursa zilizo mbele yao katika tasnia ya ubunifu.

" Mafunzo mliyoyapata kuhusu miliki-Bunifu na usajili wa haki miliki, mifumo ya biashara, namna ya kutafuta na kufungua fursa za ujasiliamali, namna ya kutafuta fedha na nyingine, yatawasaidia katika kuboresha kazi inayofanya na serikali inaamini kuwa elimu hii ni muhimu sana hasa kwa wabunifu wadogo wadogo ambao rasilimali zao ni ndogo", amesema Prof. Mdoe

Ameongeza kuwa, katika kuhakikisha kuwa ubunifu unakuwa na manufaa kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wataendelezwa kwa kuwasaidia kuandaa michoro ya utaalamu ili kuweka mawazo yao katika uhalisia huki wengine wakipatiwa vitendea kazi ili kuendelea bunifu zao.

Wito wangu kwenu ni kwamba, msaada wowote mtakaopewa tambueni kuwa umetoka na pesa za walipe kodi, ninawasihi mtumie fursa hiyo kuleta mchango chafya kwa jamii, kwani ubunifu wenu unategemewa kutatua changamoto zinazoikabili jamii na hivyo kuchangia kwenye pato la Taifa,amesema Prof. Mdoe.
 
Ameongeza kuwa, katika kuzingatia umuhimu wa bunifu, serikali ya awamu ya Tano imesema itahakikisha mchango ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unapewa kipaumbele ili kuhakikisha uchumi unaonekana na sekta hiyo unadhihirika wazi wazi.

Kwa upande wake, Mkurugezi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt, Amos Nungu amesema, magunzo hayo ni takes katika mwongozo wa Tume wa kusimamia utafiti na ubunifu ambayo ni lazima yafanyike kabla ya washiriki hao kupatiwa fedha za ufadhili .

Amesema, washiriki  wa upande wa MAKISATU ni 70 kutoka ambao ni wanafunzi wa shule za msingi, Sekondari, wabunifu katoka sekta isiyo rasmi na wabunifu kutoka vyuo vya ufundi stadium (VETA).

Ameongeza kuwa, mwaka huu Tume imepanga kuwaendeleza wabunifu hao kwa njia mbali mbali ikiwemo  kuwasaidia kuandaa michoro ya kitaalamunili kuwezesha uzalishaji wa ridhaa zai kirahisi, kuwanunulia vitendea kazi ambapo wale watakaokuwa na uhitaji watakabidhiwa na vingine vitawekwa kwenye Taasisi ili vitumike kwao na kwa wengine watakaokuja.

"Pia wapo watakaounganishwa na Taasisi ili kuwasaidia kuendelea bunifu zao na kuwasaidia kupata ulinzi wa mmiliki bunifu, amesema Dkt.Nungu Aidha Dkt  Nungu amewaasa washiriki hao kutumia fedha watakazopatiwa kwa malengo tarajiwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Professa James mdoe, wa kwanza kulia, akikabidhi mfano wa hundi  kwa uwakilishi wa watafiti, Profesa Loth Mulungu kushoto, wa Chuo cha Kilomo SUA. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu,  Dkt Amos Nungu  wakati wa warsha ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo washiriki wa Makisatu kuhusu kuendeleza bunifu zao. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe, (kushoto), akihutubia wakati wa warsha ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo washiriki wa Makisatu kihusu kuendeleza bunifu zao
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Professa James mdoe, wa kwanza kulia, akikabidhi mfano wa hundi  kwa muwakilishi mbunifu, Colman Ndetembea, mwenye shati nyeupe kushoto, na katikati ni Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu,  Dkt Amos Nungu  wakati wa warsha ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo washiriki wa Makisatu kuhusu kuendeleza bunifu zao.

Baadhi ya washiriki wabunifu na watafiti wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe,  wakati wa kufunga wakati wa warsha ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo washiriki wa Makisatu kuhusu kuendeleza bunifu zao.

No comments: