NAIBU SPIKA ATOA NENO FAINALI YA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2020
Na.Khadija Seif -Michuzi Tv
NAIBU Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt .Tulia Ackson amesisitiza Wazazi na Walezi kuchukulia tasnia ya urembo kama ajira.
Akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali na wapenzi wa mashindano ya Urembo katika Fainali ya Miss Tanzania zilizokuwa zikifanyika usiku wa kuamkia leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Dk.Tulia Ackson amesema Mara nyingi Wazazi wamekua wagumu kutoa ushirikiano kwa mabinti zao na kutambua kuwa wana vipaji vinavoweza kuzaa matunda mengi.
"Tasnia ya urembo kwa sasa imekua kiasi kubwa na imekua ikitoa ajira mbalimbali,Mfano hai Muandaaji wa Shindano hilo Basilla Mwanukuzi alikua Miss Tanzania 1998 na akaweza kuona ipo haja ya kusaidia mabinti kupitia tasnia ya urembo".
Hata hivyo Dkt Tulia ametoa rai kwa Muandaaji wa Shindano hilo kuwaendeleza washiriki ambao hawatofanikiwa kushinda .
"Naimani Warembo wote waliofanikiwa kuingia 20 wamepambana hadi kufika hapo, hivyo Muandaaji anapaswa kutimiza ndoto zao kupitia tasnia ya urembo kwani imeweza kuvumbua hata vipaji vyao vingine ambavo tusingeweza kuvijua ama kuviona".
No comments: