MWANAMKE AJIFUNGUA KUKU MKOANI KIGOMA, 'HAKUWA NA DALILI ZA MIMBA'


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MWANAMKE mmoja wilayani Uvinza mkoani Kigoma, amejifungua kuku katika kituo cha Afya  Uvinza baada ya kufika kituoni hapo akidai anapata maumivu ya tumbo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Simon Chacha ,alisema  ni kweli  tukio hilo limetokea jana  baada ya mama huyo kufika katika kituo cha Afya akiwa na Mume wake akiwa na maumivu ya tumbo baada ya muda wauguzi walitoa kuku katika sehemu ya uzazi ya Mama huyo ambapo hakuna damu zilizoendelea kutoka zaidi ya uchafu tu unaotoa harufu mbaya.

Alisema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina kwa kuwa vipimo vinaonyesha Mama huyo hakuwa mjamzito,na baada ya kutolewa kuku huyo ameendelea kutoa harufu mbaya katika sehemu hiyo ya uzazi  na alikuwa na homa ,amewamugiza mganga mfawidhi ampeleke hospitali ya Rufaa Maweni kwaajili ya uchunguzi na matibabu zaidi.

" Mama huyu haoneshi dalili zozote ya kwamba alikuwa na ujauzito cha kushangaza zaidi kiumbe hicho hakiusiani na Mfuko wa uzazi isipokuwa baada ya vipimo imeonekana mama huyo anauvimbe kwenye kizazi taarifa zisizo rasmi zinasema kwamba aliingiziwa kuku huyo na Mganga wa kienyeji, mpaka sasa tumewasiliana na vyombo vya usalama kufuatilia tukio hilo", alisema Chawote.

Kwa upande wake Mama huyo ambae hakupenda jina lake litajwe, alisema yeye alianza kujisikia maumivu tumboni na hakuwa na dalili zozote za mtu mwenye mimba ameshangaa baada ya kufika Hospitali hapo kutolewa kuku tumboni mwake jambo ambalo limemuogopesha na yeye.

Nao baadhi ya Wananchi wilayani humo, Riziki Mbonabucha alisema  tukio hilo limewashangaza sana maana halijawahi kutokea katika Wilaya ya Uvinza na kama kuna mtu anahusika na kumfanyia kitendo hicho mwenzake achukuliwe hatua iliiwe fundisho.

Alisema kazi ya waganga wa kienyeji ni kuwaondolea Wananchi matatizo na sio kuwaongezea matatizo anashangaa kuona Mganga huyo aliekosa roho ya huruma kukubali kumuwekea mwanamke kuku tumboni ni unyama unaohitajika kukomeshwa.


 

No comments: