MBUNGE LUDEWA AHAIDI MIFUKO 100 YA SARUJI, FEDHA ZA KUSAIDIA UJENZI WA KANISA
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga, ameahidi mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa kanisa katoliki parokia ya Luana pamoja na shilingi milioni mbili kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya mziki katika kanisa la Anglikana lililopo kata ya milo.
Ahadi hizo amezitoa alipotembelea makanisa hayo na kufanya ibada ambapo katika kanisa katoliki alisema mifuko hiyo ya saruji itawasili kabla ya mwezi huu kumalizika na itawasilishwa kanisani hapo.
Pia aliwasihi waumini wa kanisa hilo kuungana naye katika kuchangia ili kuweza kujenga nyumba ya Mungu iliyo bora.
"Waumini wote tinapaswa kujitoa katika kutimiza kazi ya bwana kwani ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi ya Mungu kwa moyo." alisema Kamonga.
Aidha kwa upande wa Mwenyekiti wa kamati ya ununuzi wa vyombo hivyo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Milo Robert Njavike amesema ili kuweza kupata vyombo hivyo inawapasa kugharamia Tsh. Milioni 20.
Alisema fedha hizo zitatosheleza kupata vifaa hivyo vya kisasa kabisa na kuwawezesha kuabudu na kufurahi katika nyumba ya bwana.
No comments: