BEN POL MSANII PEKEE AFRIKA MASHARIKI KUSHIRIKI BARAZA LA BIASHARA HURU AFRIKA

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

            MSANII wa Muziki wa Bongo Flava,  Behnam Paul 'Ben Pol' amekuwa msanii pekee wa Tanzania na  Afrika Mashariki kuchaguliwa kushiriki katika Baraza la Biashara huru Afrika (AfCFTA) litakalofanyika nchini Afrika Kusini.

Baraza hilo limehudhuriwa na wakuu wa nchi 55 kutoka katika nchi zote Afrika.

Lengo kuu la Baraza la Biashara huru Afrika linaloanza Januari mosi mwaka 2021 ni kuziwezesha nchi za Afrika kufanya biashara bila vizuizi.              

 Akizungumzia uteuzi huo, Ben Pol amesema anamshukuru Mungu kuweza  kupata nafasi hiyo na anajivunia kuiwakilisha Tanzania na Afrika Mashariki na kati  katika baraza la Biashara huru Afrika ambalo linafanyika leo likiongozwa na Rais wa Afrika Kusini  Cyril Ramaphosa  na  Rais Paul Kagame (Rwanda).

Aidha, amesema pia kuna wakuu wa nchi 55, watendaji wakuu (CEO's) kutoka sekta binafsi, Wanamichezo na Wadau mbalimbali kutoka Afrika.

"Januari 2021 Afrika itaanza rasmi kufanya biashara huru, yaani soko la nchi za ndani lenye watu Bilioni 1.2 na thamani ya dola trilioni 2.5 ikijumuisha mataifa 55. Huu ni wakati wa Kihistoria sana kwa bara letu. Mungu ibariki Afrika," amesema.

"Napenda kuwashukuru sana Umoja wa Afrika (AU), Hongera na Asante Afrika na  Msanii pekee Tanzania na Afrika mashariki niliyechaguliwa kushiriki baraza la biashara huru Afrika (AfCFTA)  nchini Afrika Kusini leo "amesema Ben Pol.      
                            
Pia, Ben Pol amependa kumshukuru Mungu na anajivunia kuiwakilisha Tanzania na Afrika Mashariki katika Baraza la AfCFTA (African Continental Free Trade Area) leo ijumaa 04.12.2020 nchini Afrika Kusini. Huu ni wakati wa Kihistoria kwa Afrika.


 

No comments: