WOMESA WASHEREHEKEA KUFIKISHA MIAKA TISA, WAZINDUA MRADI WAO WA CATCH THEM YOUNG




Katibu wa Asasi ya Wanawake katika sekta ya bahari ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini(WOMESA)nchini Dk.Devotha Mandanda akizungumza leo wakati wa mkutano mkuu sambamba na kuadhimisha miaka tisa tangu kuanza kwa asasi hiyo ambayo imejipatia mafanikio makubwa.


Sehemu ya wanachama wa WOMESA wakipiga makofi kama ishara ya kusherekehea miaka mita tangu kuanzishwa kwa WOMESA sambamba na kuzindua mradi wa Catch them young.


Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Chuo cha Baharia Dar es Salaam(DMI)wakiwa makini kufuatilia mkutano wa Asasi ya Wanawake katika sekta ya bahari ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini(WOMESA).

Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katondo(kushoto) akiwa Katibu wa WOMESA Dk.Devotha Mandanda kabla ya kuzindua mradi wa mradi wa Catch them young.

Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katondo akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano mkuu wa WOMESA ambapo amezindua rsmi mradi wa Catch them young unaolenga kuwandaa wanafunzi walioko shuleni kuanza kuweka mkazo katika sekta ya ubaharia.

Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katondo(wa pili) aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu na maadhimisho ya miaka tisa tangu kuanzishwa kwa WOMESA akiwa makini kufuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi.

Mwanamke wa kwanza kuwa baharia nchini Tanzania Mhandisi Regina Mbilinyi(wa pili kulia) akiwa na wanachama wa WOMESA wakati wa mkutano mkuu sambamba na maadhimisho ya kutimiza miaka mita tangu kuanzishwa kwa WOMESA.

Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katondo(kulia) akiwa ameshikana mkono na Mwalimu wa DMI Nyamizi Mgawe(kushoto).

Mgeni rasmi Stella Katondo (wa tatu kushoto) pamoja na wadau wa sekta ya Bahari wakiwemo viongozi wa WOMESA wakiwa na wanafunzi wanaosoma Chuo cha Baharia Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka tisa tangu kuanzishwa kwa WOMESA.

Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katondo(wa tatu kushoto) na viongozi wa WOMESA wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kike(waliosimama nyuma) ambao wana ndoto za kuwa mabaharia.

Katibu wa Asasi ya Wanawake katika sekta ya bahari ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini(WOMESA)nchini Dk.Devotha Mandanda(kushoto) akikabidhi zawadi waliyoitoa kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katondo(kulia).

Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katondo(kulia)akimkabidhi tuzo Nohodha Feruz Kassim Feruz ambaye ni Meneja Operesheni wa Kampuni ya Azam Marine(kushoto).Tuzo hiyo inatokana na WOMESA kutambua mchango wa kampuni hiyo katika sekta ya bahari nchini.




Na Said Mwishehe, Michuzi TV

ASASI ya Wanawake katika sekta ya bahari ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini(WOMESA) imefanya mkutano wake mkuu sambamba na kuadhimisha miaka tisa tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika leo Novemba 27 , 2020 jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katondo amewapongeza WOMESA kutokana na mafanikio ambayo wameyapata kwa nyakati tofauti.

Amefafanua WOMESA imeasisiwa na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya Bahari(IMO) chini ya kitengo chake cha masuala ya jinsia."Lengo kuu la WOMESA pamoja na asasi nyingine zenye malengo kama WOMESA , ni kuchochea usawa wa kujinsia katika sekta ya bahari.

"Hii inatokana na ukweli usioficha kwamba kuwekeza kwa mwanamke ni njia bora zaidi ya kuiinua jamii , mashirika na mataifa kwa ujumla.Kukiwa na usawa wa jinsia hata uchumi wa nchi utastawi, utafiti unaonesha mashirika yenye watendaji wengi wanawake yako vizuri kimaendeleo ukilinganisha na mashirika yenye wanawake wachache.

"Makubaliano ya amani yanayoshirikisha wanawake ni bora zaidi, mabunge yenye idadi ya wanawake wengi yanatunga na kupitisha sheria za masuala muhimu ya kijamii.Hivyo ni ukweli usiopingika WOMESA ikitembea kwenye malengo yake itakwenda kuinua sekta yetu hii ya bahari nchini Tanzania,"amesema.

Ameongeza amesikia hotuba ya WOMESA ambavyo imesheheni mafanikio na jitihada zilizofanyika na zinazoendelea kufanyikakwa ajili ya kufikia malengo yake iliyojiwekea.

Na kwamba mradi wa 'Catch them Young' ambao ameuzindua leo ni moja ya hatua muhimu imechukua katika kuleta uwiano wa jinsia pamoja a kutangaza fursa zilizopo kwenye sekta hiyo.

"Jitihada hizi mnazozifanya ni kilelezo cha kuinua uchumi wa bahari, nawaomba WOMESA waendelee kuelekeza nguvu zaidi katika kuinua uwiano wa wasichana katika fani ya ubaharia kwani idadi yao iko chini ukulinganisha na wavulana katika fani hiyo.

"Zipo takwimu zinaoneshana idadi ya baharia wanawake duniani ni asilimia mbili tu ya mabaharia milioni 1.2 duniani.Ni matumaini yangu mradi wa Catch them Young pamoja na programu ya Mentorship ambayo imekuwa endelevu sasa italeta matokeo chanya na idadi ya vijana wa kike itaendelea kuongezeka katika vyuo vyetu vinavyotoa elimu ya bahari.

"Niwahakikishie Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iko bega kwa bega nanyi na inaunga mkono jitihada zinazofanywa na WOMESA.Nawaongeza WOMESA kwa kufanikisha mkutano huu, najua muda wa miaka tisa ambao umekuwepo kama mtoto basi alikuwa anaelekea kumaliza elimu ya msingi,"amesema Katondo.

Awali Katibu wa WOMESA Tanzania , Dk.Devotha Mandanda ametumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio lukuki ambayo wameyapata na mikakati yao ni kuendelea kuweka mipango na mikakati ambayo itawafanya waendelee kupiga hatua zaidi.Amezungumzia namna ambavyo wanachama wa WOMESA wanavyopata fursa mbalimbali zikiwemo za kuendelezwa kielimu katika masuala yanayohusu sekta ya bahari.

Aidha amezungumzia mkakati wa kuendeleza vijana wa kike wa kuwaandaa mapema ili waje kuwa mabaharia na katika kufanikisha hilo wamezindua mradi wa Catch them Young ambao ni mahusi kabisa katika kufuata wasichana walioko shuleni na kisha kuanza kuwaandaa.

No comments: