Wananchi wafurika kupata huduma za upimaji afya katika maadhimisho.
*NHIF yaendelea kutoa elimu umuhimu wa wananchi kuwa na Bima ya Afya.
Na Ripota Wetu,Michuzi TV
Wananchi wamesema utaratibu wa upimaji wa afya ufanyike Mara kwa mara kwa kuwa na huduma za pamoja kwani kutasaidia wananchi kujua afya zao.
Wamesema katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza ni changamoto ya makundi mbalimbali katika afya ikilinganishwa na miaka nyuma iliyopita.
Akizungumza na Michuzi Blog mwanachi Joseph Marco amesema kuwa kwa sasa makundi ya vijana yako kwenye changamoto ya Magonjwa yasiyoambukiza kutokana na ulaji usiozingatia,Lishe pamoja na kutofanya mazoezi.
Amesema changamoto nyongine ni tatizo la macho huku akisema watu wanamatatizo ya kuona na foleni imekuwa kuwa kubwa.
Nae mwanaisha Abeid amesema kuwa serikali imeweka utaratibu mzuri wa kuadhimisha na kuweka huduma zote za upimaji wa afya.
Afisa Udhibiti Ubora wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt.Baraka Nathael akitoa elimu kuhusiana na Mfuko huo na umuhimu wa wananchi kuwa na Bima ya Afya ya kuweza kumfanya mwananchi kuwa na uhakika wa afya yake wakati wa utoaji huduma kwa wananchi katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yanayoendeleo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika gari wakisubiri kufanya vipimo katika gari hilo katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yanayoendeleaa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
No comments: