Walimu,wasimamizi Waonywa kushiriki rushwa kwenye mitihani


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Walimu na Wasimamizi wa Mitihani Mkoani Njombe Wametakiwa kuacha kushiriki Vitendo Vinavyo ashiria Utoaji wa Rushwa katika Kipindi Cha Mitihani ya Kidato Cha nne na Chapili inayotarajiwa Kufanyika Siku za Usoni Hapa nchini.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Ruswha (Takukuru) Mkoa wa Njombe Kassimu Efreim Wakati Tasisi hiyo ikitoa Elimu kwa Club za Wapinga Rushwa Zilizoundwa Katika Mashule mabalimbali Mkoani hapa Zenye Lengo la Kukemea Vitendo Vya Rushwa.

"Tunaomba sana wasiamizi wa mitihani zingatieni sheria kanauni na taratibu wa usimamizi wa mitihani ya serikali ,tunategemea kusiwe na ushawishi wa rushwa na takukuru tupo"alisema Kassimu Efreim

Mwalimu Sreven David Mwakila Kutoka Mpechi Sekondary Pamoja na Mwalimu Adbelta Mgaya wanasema kuwa Wamekuwa Wakitoa Elimu kwa Wanafunzi juu ya Madhara ya Rushwa huku Wakitaja Madhara Yenyewe na Namna yanavyoathiri Jamii.

"Tunaweza tukapata wataalamu ambao hawajakizi vigezo lakini vile vile uchumi wa taifa unaweza ukadidimia mfano zikajengwa barabara mbovu na mwisho wa siku zikaharibika,kwa hiyo sisi kama walimu tumejifunza mengi na tutawaambia wenzetu kwamba rushwa ina atahari kubwa sana kwa taifa letu"

Je?Wanafunzi Wenyewe Wanaelewa Nini Kuhusu Madhara Ya Rushwa katika Jamii na Hata katika Kipindi Cha Mitihani.

"Kwa kweli tunapata elimu kuhusu madhara ya rushwa kwa njia mbali mbali kwa mfano watu wa Takukuru kufika shuleni kwetu lakini pia matamasha mbali mbali,na rushwa ina atahari nyingi mfano kupata wataalamu wasiokidhi vigezo"walisema baadhi ya wanafunzi

Rushwa ni Adui wa Haki,Serikali,Wadau mbalimbali Wamekuwa Wakikemea Vitendo Vya bRushwa Ili Kuweka Usawa katika Jamii Baina ya Mwenye Nacho na Asie Nacho.

Kassimu Efreim Mkuu wa Takukuru mkoa wa Njombe akizungumza na wanafunzi wa Club za Wapinga Rushwa Zilizoundwa Katika Mashule mabalimbali mjini Njombe

Baadhi ya wanafunzi wakiwa makini kusikiliza elimu kutoka TAKUKURU
Walimu wakiwa makini kusikiliza ofisa wa takukuru juu madhara ya Rushwa.

No comments: