Wakulima wa Karosho mikoa ya kusini waendelee kuhudumia na kuvuna korosho---TARI


Na Mwaandishi wetu Mtwara

TAASISI ya Utafiti wa kilimo nchini (TARI) imewashauri wakulima wa korosho mikoa ya kusini kuendelea kuhudumia mikorosho yao na kuokota korosho zinazokomaa na kuanguka hata baada ya msimu wa korosho kuisha.

Kaimu Makurungezi wa Kituo cha TARI Naliendele Daktari Fortunus Kapinga ametoa ushauri huo hapa kutokana na mikorosho katika baadhi ya maeneo kuanza kustawi na maua kuchipua upya, hali inayoashiria uwepo wa kukua kwa korosho zaidi hata baada ya msimu huu kuisha.

Kapinga amesema kwamba maua hayo yameanza kuchipua upya kwa wingi kutokana na uwepo wa hali ya hewa nzuri ambayo imepelekea mikorosho hiyo kustawi na kutoa maua.

Amesema hali hiyo imejionyesha zaidi katika maeneo ambayo awali yalikubwa na tatizo la kukauka kwa maua ya mikorosho kwa sababu ya baridi iliyotokana na kushuka kwa joto chini ya sentigrade 20 hadi kufikia nyuzi joto sentigrade 17 kuanzia mnamo mwezi Julai hadi Agosti mwaka huu.

Maua ambayo yalikauka kipindi cha baridi yalianza upya kuchipuka  kati ya mwezi tisa na kumi baada ya kurejea kwa hali ya hewa kati ya sentigredi 20 na 30 na kuruhusu kustawi kwa mikorosho na maua kuchipua.

Kapinga amesema hali hiyo huenda wakulima wakaona sio ya kaweida na wengi wakaacha kuhudumia mikorosho yao na kuacha korosho nyingi shambani kwa kudhani kuwa msimu wa korosho umaisha.

Amesema wakulima wengi wamezoa kuacha kuokota korosho ifikapo mwezi wa kumi na mbili kwa dhana kwamba msimu umeisha na kuongeza kuwa wakulima hao waendelee kuhudumia mashamba yao kadri maua yanapoendelea kuchipue na kutoa korosho.

 “Wakulima wakiona mikorsoho inatoa maua hawana haja ya kuogopa wala kushangaa, kwama ni kiti cha ajaabu, hapana, ni hali ya hewa ambayo kwa mwaka huu imefanya mikorosho iweze kuonyesha tabia kama hizo,” amesema na kuongeza kuwa wakulima wanaweza kuendelea kuhudumia mikorosho na kutunza maua ambayo yanaendele kuchipuka na ambayo yamechipuka na kutoa korosho.

Ameongeza kuwa mikorosho haswa inayotokana na mbegu bora huwa ina kaweida ya kufidia uzao wa korosho ambazo hushindwa kukua vizuri kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushuka au kupanda kwa hewani zaid ya nyuzi joto 30.

Wakizungumzi hali hiyo, wakulima wa korosho mkoani Mtwara wamekili na hali kushuhudia hali hiyo ya maua kuchipua huku wakidai kuwa sio kaweida kama walivyozoea.

Katika msimu wa 2020/2021, Bodi ya korosho nchini (CBT) ilitangaza mategemeo ya kupata mavuno ya korosho tani 278,000  ilikinganishwa na mwaka juzi 2018/2019 ambapo ilikuwa ni  tani 225,000 na mwaka jana 2019/2020 tani 232,000.

 

 Wahudumu wa shamba la mfano la Kituo Cha TARI Naliendele wakielezea jinsi maua hayo yalipoanza kuchipuka na kiendelea Hali ambayo limejitokeza tofauti na misimu mingine ya nyuma. 
KAIMU MKURUNGEZI WA kituo cha TARI Naliendele Daktari Fortunus Kapinga akionyesha wanahabari maua ya korosho ambayo yanachipuka kutokana na Hali ya hewa kuwa nzuri na kupelekea kuchipuka na kustawi kwa maua ya korosho katika shamba la kituo hicho Cha TARI Naliendele

No comments: