Wabunge wa CCM Hawapingi Miradi ya Maendeleo – Masauni
Mbunge mteule wa Kikwajuni (CCM), Mhe. Hamad Yussuf Masauni amesema wabunge wanaotokana na CCM ndio waliokua wakitoa michango iliyoisaidia Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo wananchi wapuuze propaganda za wapinzani zinazodai eti Bunge la 12 halitaikosoa Serikali.
Mhe. Masauni ameyasema hayo leo alipozungumza na mwandishi wa habari hii kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
“Hata katika bunge lililopita michango mingi iliyokua ikiisaidia Serikali ni ya wabunge wa CCM, wabunge wa CCM hawasusii bajeti, wabunge wa CCM hawatoki nje wakafunga midomo yao, wabunge wa CCM hawapingi miradi ya maendeleo au leo hawasemi hiki kesho wakasema kile, wana misimamo isiyoyumba”, alisema Masauni.
Naye mbunge mteule wa Ukonga (CCM), Mhe. Jerry Slaa amesema kabla ya mfumo wa vyama vingi, Bunge la wakati huo lilikua na wabunge wanaokosoa kwa kujenga hoja na kujadili maendeleo ya majimbo yao.
“Katika utafiti wangu kupitia hansard za bunge, bunge la chama kimoja lilikua la moto kuliko bunge la vyama vingi, moto wake ulikua unatokana na hoja nzito za maswala ya kitaifa lakini wabunge walikua na misimamo mikali sana ya mambo yanayohusu maendeleo ya majimbo yao”, alisema Slaa.
Sambamba na hayo, mbunge mteule wa Mtwara Mjini (CCM), Mhe. Hassan Mtenga amesema atahakikisha anawatumikia wananchi waliomtuma.
“Sisi tumetumwa na wananchi kama kuna hoja isiyo nzuri tutaikosoa, kabla ya mfumo wa vyama vingi kulikua na wabunge wa CCM wanaoikosoa sana Serikali, kwetu Mtwara alikwepo mzee Nandonde ambaye alikua a
kikosoa Serikali” alieleza Mtenga.
No comments: