VYETI VYA KUZALIWA KUTOLEWA MARA TU MTOTO ANAPOZALIWA KUFIKIA MWAKA 2022



Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu Bi Emmy Hudson akipokea magari mawili aina ya Land cruiser hardtop yenye thamani ya Tshs Milioni 240 yaliyotolewa na Serikali ya Canada kupitia Shirika la kuhudumia Watoto Duniani UNICEF ili kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa usajili wa vizazi na vifo nchini.wa kwanza kulia ni 
Meneja wa ugomboaji na uondoshaji wa mizigo ya Serikali GPSA Ndugu. Jimmy Abdiel, wengine ni Mkurugenzi wa Huduma na Biashara ndugu Charles Salyeem(kulia kwake) na Meneja Ununuzi 
 Ndugu. Wilfred Masanja(wa kwanza kushoto)
Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu Bi Emmy Hudson (kulia) akipokea magari mawili aina ya Land cruiser hardtop yenye thamani ya Tshs Milioni 240 yaliyotolewa na Serikali ya Canada kupitia Shirika la kuhudumia Watoto Duniani UNICEF ili kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa usajili wa vizazi na vifo nchini.


*RITA yapokea Msaada wa Magari mawili kusaidia usajili wa watoto

*RITA yangara katika Usajili wa Vizazi kwa watoto Barani Afrika

*Huduma za usajili zasogezwa karibu na makazi ya wananchi

IMEELEZWA kuwa, hadi kufikia mwaka mwaka 2022 watoto wote wanaozaliwa nchini watakuwa wanapata vyeti vya kuzaliwa mara tu wanapozaliwa kutokana maboresho makubwa katika mfumo wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu hasa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto kupitia Mpango wa Usajili wa Watoto walio na Umri Chini ya Miaka Mitano (Under-Five Birth Registration Initiative) umeanza na unaendelea kutekelezwa katika mikoa 18 nchini na kufikia mwaka huo Utekelezaji katika mikoa 8 iliyobaki utakuwa umekamilika.

Mpango wa usajili wa watoto umewezesha kugatua majukumu ya usajili na kusogeza huduma hiyo karibu na makazi ya wananchi ambapo huduma za usajili kwa sasa zinatolewa BILA MALIPO katika vituo vya Tiba na Ofisi za Watendaji Kata. Maeneo hayo ni ya kimkakati  kwani ni rahisi kwa kila mwananchi kufika na kupatiwa huduma husika. Mtoto anayezaliwa katika kituo cha Tiba anaweza kupata cheti cha kuzaliwa kabla ya kutoka hospitali cha msingi ni kwamba wazazi wawe wameshaanda jina la mtoto litakalojazwa katika cheti.

Mikoa ambapo zaidi ya watoto Milioni 5.2 wameweza kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa hivyo kuongeza kiwango cha usajili ya watoto wa kundi hilo kutoka asilimia 13 Mwaka 2012 mpaka kufikia asilimia 49.4 Mwaka 2020. 

Nimepokea msaada wa magari mawili mapya aina ya Toyota Landcruiser yenye thamani ya TShs Milioni 240 yaliyotolewa na Serekali ya Canada kupitia Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kwa ajili ya kuimarisha usimamizi na ufatiliaji wa Mpangu huu na RITA tunaamini yataongeza ufanisi kwa watendaji wa Wakala kwani yatawezesha watendaji kufika mpaka maeneo ambayo ni magumu kufikika hivyo kuongeza kasi katika kufikia malengo.

 “Kwa niaba ya Serekali, napenda kuwashukuru Wadau wa Maendeleo ya magari waliyotupatia na yamekuja katika wakati sahihi kwani Idadi ya mikoa ambayo tunatekeleza mpango huu imeongezeka hivyo kuhitaji vitendea kazi vingi zaidi ili kuhakikisha majukumu yanaendelea kutekelezwa kikamilifu”.

Tanzania imechaguliwa na Umoja wa Afrika (AU) kuwa kati ya nchi tano (5) za Bara la Afrika zitakazoongoza Kampeni ya kuongeza kasi ya Usajili wa Vizazi kwa Watoto Barani Afrika inayojulikana kama “Bila kuwa na Jina; Utambulisho wa Kisheria kwa kila mtoto; Upatikanaji wa haki kwa kila mtoto” ambayo inaendeshwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Umoja wa Afrika (AU).

Tanzania imechaguliwa kutokana na mafanikio iliyoyapata miaka ya karibuni katika kuongeza kasi ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu hasa usajili wa vizazi kwa watoto. Sababu nyingine zilizoainishwa ni pamoja na nchi kuwa na utashi wa kisiasa katika masuala ya usajili wa vizazi na kutekeleza kikamilifu kanuni muhimu zinazounga mkono kampeni hii.

 Tunawaomba wadau zaidi kuendelea kushirikiana na Wakala katika kuhakikisha mpango huu unaendelea kuwasaidia watoto kupata haki yao ya msingi ya kutambuliwa kwani Rasilimali zaidi zinahitajika hasa katika hatua za kuhakikisha huduma zinakuwa endelevu.


No comments: