VIONGOZI WA DINI WAOBWA KUWEKA MKAZO KATIKA KUSIMAMIA MAADILI YA JAMII
Mkuu wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda wa pili kulia akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya umoja wa viongozi wa dini Karatu ,juzi Mara baada ya kufungua semina ya kamati ya umoja ya viongozi wa dini inter faith uliofanyika ukumbi wa KKKT Karatu (picha na Woinde Shizza ,ARUSHA)
Na Woinde Shizza , Michuzi TV Arusha
VIONGOZI wa dini waombwa kuweka mkazo katika kusimamia maadili ya jamii, ili kupunguza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na upotevu wa maadili ambavyo vimezidi kukithiri katika jamii.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda wakati akifungua semina ya kamati ya umoja ya viongozi wa dini Inter Faith
Alisema serikali ina amini sana viongozi wa dini katika kujenga jamii yenye hofu ya Mungu, changamoto ya upotevu wa maadili inasababisha watoto kutaabika na imeongeza watoto wanaoishi katika mazingira magumu ni vyema wawaambie na wabadilishe nafsi zao watu hao na kuwaambia kwamba mambo wanayoyofanya hayampendezi Mwenyezi Mungu.
Kayanda alipongeza wazo la kuwa na kamati ya umoja wa viongozi wa dini (Inter Face) na kusema umoja huo utasaidia serikali katika mazoezi ya kitaifa kama chanjo, kusaidia kuhamasisha wananchi,umoja wa viongozi wa dini Inter Face utasadia kuleta wananchi pamoja.
Sambamba na hayo Kayanda aliwashukuru viongozi wa dini kwa kuombea amani ya nchi kipindi cha uchaguzi na kusema wamemaliza uchaguzi salama hakuna vita wala hakuna ogomvi hili ni jambo la kujivunia.
Aliongeza kuwa uchaguzi Mkuu umeisha lazima wananchi tuungane na tuwe kitu kimoja na tushiriki katika shughuli za maendeleo ,kwani Maendeleo ya wana Karatu yataletwa na wana Karatu wenyewe na si mtu nje ya Karatu.
Kayanda ameomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani na kuitunza, kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya nchi , nakubainisha kuwa amani ni tunu ya kipekee, hatuwezi kujenga hospitali kujenga barabara au kununua ndege kama amani itatetereka.
Aidha alitumia nafasi hiyo kupongeza kamati ya umoja wa viongozi wa dini Inter Face kwa miradi mbalimbali wanayosimamia kwa ajili ya kusaidia jamii.
Akitoa neno la shukrani Padre Pamphili Nada alisema viongozi wa dini wataendelea kuhubiri amani kwa kundi kubwa la waumini ambalo liko nyuma yao, na kubainisha lazima mwanadamu apate maendeleo ya kweli ya roho na mwili, amani ikitoweka basi hakuna kitakachowezekana.
Alisema ni vyema tumshukuru Mungu tumepata Rais makini mwenye maono, ujasiri wake umetuvusha kwenye changamoto ya korona ,ambapo pia viongozi wa dini kwa pamoja wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali wakati wowote.
No comments: