UKARABATI JENGO LA WATOTO WACHANGA HOSPITALI YA MJI KAHAMA WAKAMILIKA

 

Wodi maalum kwa ajili kulazwa watoto wagonjwa kwenye Jengo la Watoto wachanga la Hospitali ya Mji Kahama ambalo ukarabati wake ukamekamilika tayari kuanza huduma baada ya mkandarasi kukabidhi jengo hilo.

Wodi maalum kwa ajili kulazwa watoto njiti kwenye Jengo Watoto la wachanga la Hospitali ya Mji Kahama ambalo ukarabati wake ukamekamilika tayari kuanza huduma baada ya mkandarasi kukabidhi jingo hilo.

Ujenzi wa Jengo la Upasuaji ukiendelea katika hatua za Mwisho jengo hili liko mkatika Hospitali ya Jakaya Kikwete iliyoko Kishapu Mkoani Shinyanga.

***************************************

Na Anthony Ishengoma- SHINYANGA

Serikali Mkoani Shinyanga imekamilish ukarabati wa Jengo la watoto wachanga lenye thamani ya sh. 103 Mil. la Hospitali ya Mji Kahama pamoja na kuweka vifaa kwa ajili ya kuhudumia watoto njiti na ICU ya  watoto wanaohitaji uangalizi maalum.

Ufadhili wa fedha za  ukarabati wa Jengo hilo zimetolewa na Shirika la Kimataifa Touch Foundation ambalo pia linafadhili ujenzi wa Majengo ya Upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Kishapu, Kituo cha Afya Lunguya na Burungwa vyote vya  Halmashauri ya Ushetu na Msalala Wilayani Kahama  Mkoani Shinyanga.

Akiongea wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Majengo hayo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile alisema kuwa ukarabati wa Jengo la Watoto Wachanga umekamilika na  vifaa tayari vimekabidhiwa kwa ajili ya kupangwa  na  kuanza kufanya kazi na kuongeza kuwa  ujenzi wa majengo ya upasuaji uko katika hutua za mwisho kukamilika.

Aidha Dkt. Ndungile ameongeza kuwa baadhi ya Wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Mji Kahama tayari wamepelekwa katika hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kujifunza namna bora ya kutumia vifaa hivyo tayari kwa kuanza kutoa huduma kwa kutumia vifaa vipya vya matibabu ya watoto vilivyopo katika Jengo hilo.

Naye Muhandisi wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Francis Magoti aliongeza kuwa kwasasa shirika la kimataifa la Touch Foundation kupitia ufadhili wake limewezesha ujenzi Jengo la Kisasa Kabisa la Upasuaji katika Hospitali ya Jakaya Kikwete iliyoko Kishapu Mkoani Shinyanga akiyataja pia majengo mengine ya Runguya na Burungwa kuwa yanajengwa kuzingatia vigezo vya Wizara ya Afya.

Aidha Muhandisi Magoti aliongeza kuwa Jengo la Watoto Wachanga la Hospitali ya Mji Kahama lilikuwa limechakaa sana na sasa limekarabatiwa na kuongeza wodi ya watoto njiti na wodi ya uangalizi maalumu ya watoto wagonjwa (ICU) akilitaja Shirika la Touch Foundation kwa kufanikisha ukarabati huo kwa gharama ya Sh. Milioni 103.

Wakati huohuo Mwanazengo kutoka Kijiji cha Burungwa Bw. Dominic Otieno amepongeza juhudi za Serikali kwa kuanza ujenzi wa Jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Burungwa na kusema kuwa Jengo kama hilo la awali ni dogo sana hivyo ujenzi wa wa Jengo jipya ni furasa tosha kwa huduma za mama na mtoto.

Shirika la Touch Foundation sio tu linafanya ukarabati katika na ujenzi majengo ya huduma za mama na mtoto lakini pia Shirika hilo linafadhili pia huduma ya usafiri kwa akina mama wajawazito wanaohitaji kujifungua lakini wako katika maeneo ambayo ni vigumu kupata usafiri wa haraka kuwapeleka katika vituo vya Afya katika Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Path Foundation kupitia mradi ujlikanao kama M-Mama.   

No comments: