TOTAL TANZANIA YAJIVUNIA MAFANIKIO YA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA
KAMPUNI ya Mafuta ya Total Tanzania imesema kuwa wateja wao wamekuwa bega kwa bega katika kuwaunga mkono na bidhaa zao na huduma wanazozitoa hivyo sio wateja wamekuwa wadau.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Jean-Francois Schoepp wakati awamu ya Pili ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika Kituo cha Mafuta cha Total Africana Mbezi Beach amesema kuwa kutokana mafanikio makubwa na mrejesho chanya awamu ya kwanza wa wiki maalum ya Huduma kwa Wateja ya Total iliyofanyika Novemba 2019 na kufanya kampuni kurudi tena kwa awamu ya pili ya wiki ya huduma kwa wateja inayolenga kuweka msisitizo wa kujenga mahusiano bora na ya kudumu kwa Wateja.
Amesema kuwa Total kwa mwaka huu imejikita katika katika kutimiza ahadi zake kwa Wateja wake wote biashara mtandaoni na Biashara kwenda biashara nyingene(B2C&B2B) kwa kuweka mazingira bora ya kufanya biashara kwa kuwa wasikivu zaidi kwa Wateja kwa kuandaa hafla maalum zinazowalenga Wateja na fursa kwa Total Tanzania kuelezea kwa vitendo kuwa wanawasikiliza na kuwapa kipaumbele Wateja.
Schoepp amesema huduma kwa wateja inatoa fursa kwa kampuni kuelewa zaidi changamoto za wateja pamoja na matarajio yao kutoka kwetu ili kuweza kuwapatia bidhaa na huduma zitazokidhi mahitaji yao .
"Total tunaamini na kutambua kuwa wateja wetu ni zaidi ya wateja na washirika wetu .Wao ndio chanzo Cha biashara na mafanikio ya Total nchini hivyo tunawashukuru sana kwa kuendelea kutuunga mkono na kutuamini na tunawakaribisha wote kutupa mawazo nanmaoni yenu juu ya Huduma zetu tupate kuboresha na kuwapa huduma Bora zaidi." Amesema Schoepp.
Aidha amesema kuwa awamu ya pili ya wateja ya Total imekuwa ya mafanikio sana kutokana na jitihada za wafanyakazi wa Total hivyo tutaendelea kuwa pamoja na wateja.
No comments: