TCRA YAIPIGA RUNGU LA MILIONI 9 PASSION FM
*Ni kutokana na mtu kutangaziwa umbea bila yeye kuzungumza.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV.
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipiga kituo cha Passion FM Radio faini ya sh.milioni Tisa baada ya kutangaza stori za Umbea mtaani.
Imedaiwa Kituo cha Radio hiyo kilitangaza stori inayomhusu Khadija Ally bila kufuata kanuni za utangazaji na kumfanya kutokuwa ushirikiano na wajamii.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Valerie Msoka amesema kuwa Kituo Passion FM Radio kilitoa Habari ya Bi. Khadija Ally ya kuwa Mtaa wa Kimwani Chanika Mwisho ya kutaka kumhamisha bi Khadija Ally kutokana na umbea kupitia mkutano wa wananchi na Kituo hicho hakikuweka mazungumzo bi khadija.
Katika mkutano huo yalizungumzwa masuala mbalimbali ikiwemo Suala Umbea na Mambo mengine bila kutajwa jina la Mtu wa kufanya Umbea.
Msoka amesema kuwa Kituo hicho kilitakiwa kuweka upande wa Pili kutokana na kutuhumiwa kwa Bi Khadija kwa ajili ya Umbea.
Licha ya kulipa faini hiyo pia wanatakiwa kumuomba radhi bi Khadija Ally mara tatu kwa muda wa siku tatu itakayoishia Novemba 16 pamoja na kuomba radhi hiyo mara tatu katika kipindi cha Jogoo.
Kamati hiyo imesema Kituo cha Passion FM Radio hawako makini katika usimamizi wa vipindi vyao pamoja kukosa weledi wa usimamizi wa kuzingatia kanuni za maudhui ya utangazaji.
Hata hivyo amesema kuwa kama hawajaridhika na hukumu hiyo wanaweza kukata rufaa ndani ya Siku 30.
No comments: