TAHADHARI YA MVUA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua kubwa Inatarajiwa kunyesha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Jumapili Novemba 8, 2020.
Katika Utabiri wao, TMA imesema mvua zinatarajiwa kunyesha katikati mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro,Tanga, visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Zinatarajiwa kuanza leo hadi Novemba 10, 2020 na kwamba inatarajiwa maeneo hayo yatakuwa yenye tahadhali kubwa hususani leo na kesho ambapo vipindi vikubwa vya mvua vinatarajiwa kujitokeza
Aidha TMA wamesema, athari mbali mbali zinaweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na mafuriko kwenye makazi ya watu, baadhi ya barabara kufungwa na shughuli za kiuchumi kusimama.
No comments: