SUTI ZATAWALA WABUNGE WAKIINGIA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA
Charles James, Michuzi TV
NI mwendo wa sauti! Hii ndio kauli unayoweza kusema baada ya leo wabunge waliochaguliwa na wananchi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuripoti bungeni leo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibunge.
Michuzi Blog imeshuhudia kundi kubwa la wabunge wakiingia katika viwanja vya Bunge wakiwa wamevalia Suti zao nadhifu za aina mbalimbali.
Akizungumza na Michuzi Blog Mbunge wa Mlimba mkoani Morogoro (CCM), Godwin Kunambi amesema licha ya kuwa ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni lakini amejipanga kuhakikisha anafanya kazi yake ya kuisimamia serikali na kuwatetea wananchi wake wa Mlimba waliomchagua kwa kufuata Katiba, Sheria, Kanuni na Miongozo ya Bunge.
Nae Patrobas Katambi mbunge wa Shinyanga Mjini amesema anaamini wingi wa wabunge wa CCM utasaidia kuisimamia serikali katika kuwatumikia wananchi wake.
Shughuli kubwa katika siku ya leo ni kumchagua Spika wa Bunge na kuwaapisha Wabunge tayari kwa kuanza kuwatumikia wananchi.
Utatu wa Kazi! Wabunge wa CCM kutoka kulia ni Nape Nnauye wa Jimbo la Mtama, Dotto Biteko wa Jimbo la Bukombe (katikati) na Hussein Bashe wa Nzega Vijijini.
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Manyara, Asia Kilangi akiingia kwenye viwanja vya Bunge asubuhi ya leo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kulia), Patrobas Katambi na Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigonga wakiingia kwenye viwanja vya Bunge mapema asubuhi ya leo.
Mbunge Mteule wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro CCM akiingia katika viwanja vya Bunge tayari kuanza shughuli zake za kibunge.Mbunge Mteule wa Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi (kulia) akiwa na Mbunge Mteule wa Ubungo, Prof Kitila Mkumbo nje ya viwanja vya bungeni mapema leo asubuhi.
No comments: