RC Arusha ataka kampuni za Utalii na mahoteli kupunguza bei kwa Watalii wa ndani
Na Woinde Shizza , Michuzi TV Arusha
MKUU wa mkoa wa Arusha, Idd Kimanta amewataka wamikili wa kampuni za Utalii na mahoteli mkoani Àrusha kupunguza bei ili kuvutia Watalii wa ndani kutembelea hifadhi za Taifa.
Akizungumza na Wafanyakazi 80 wa benki ya CRDB ambao wametoka jijini Dar es salaam kuelekea mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kutalii, juzi Kimanta alisema gharama kubwa kutembelea hifadhi kunapunguza Watalii wa ndani.
"Wakati huu Taifa linakabiliwa na upungufu wa Watalii kutoka nje ni vizuri wenye kampuni za Utalii mtusaidie kushusha gharama za magari, chakula na kulala hifadhi Watalii wa ndani"alisema
Awali Mkurugenzi wa masoko wa Bodi ya Utalii nchini(TTB)Mindi Kasiga alisema Bodi hiyo kwa kushirikiana na CRDB wameweza kuanzisha kampeni za kuhamasisha Utalii wa ndani.
"Kampeni hii ya tembelea Mbuga zetu pia inahusisha shirika la ndege nchini(ACTL) kampuni ya Zara Tours na Mamlaka ya viwanja vya ndege." Alisema
Afisa Masoko Mkuu wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Michael Makombe alisema Wafanyakazi hao wa CRDB hawatajutia muda na gharama za kutembelea Ngorongoro kwani kuna vivutio vingi.
"Wakiwa Ngorongoro watashuhudia wanyama wakubwa Tembo,Simba,Nyati ,Faru wakiwa katika eneo la Creta." Alisema
Alisema pia watajionea maajabu ya Ngorongoro ikiwepo mchanga unaotembelea,makumbusho ya Olduvai na kreta ya Embakai.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Utalii(TATO), Sirili Ako alipongeza CRDB kwa kuanzisha utaratibu kupeleka Wafanyakazi hifadhini na ametaka taasisi nyingine kuiga ili Wafanyakazi waone utajiri wa Maliasili za Taifa na kuokoa sekta ya utalii.
Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega Akizungumza na Wafanyakazi 80 wa benki ya CRDB ambao wametoka jijini Dar es salaam kuelekea mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kutalii, juzi nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha walipopita.
(Picha na Woinde Shizza,ARUSHA)
No comments: