RAIS DKT. MAGUFULI AWASHUKURU VIONGOZI WA DINI

 RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi na waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wa dini nyingine nchini kwa kuliombea Taifa katika kipindi cha miaka mitano ya awamu ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano na amewasihi waendelee na utaratibu huo.

Kauli hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Novemba 27, 2020) b
aada ya kuswali swala ya Ijumaa katika msikiti wa Msalato jijini Dodoma. “Wakati najiandaa kuja kuswali nilimuaga Mheshimiwa Rais na ameniagiza nilete salamu zenu kwamba anawashukuru sana kwa kumuunga mkono.”

Waziri Mkuu amesema: “Rais Dkt. Magufuli amesema mbali na viongozi hao na waumini kumuunga mkono katika awamu ya kwanza ya uongozi wake, pia walitoa ushirikiano mkubwa katika kipindi cha kampeni kwa kuendelea kuliombea Taifa hadi uchaguzi ukafanyika kwa amani.”

Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli amewaomba viongozi hao wa dini pamoja na waumini waendelee kuliombea Taifa na viongozi wake ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa amani na utulivu.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao waendelee kuwahamasisha waumini washiriki ibada mbalimbali kwa sababu jambo hilo ni muhimu na linapaswa kufanyika kwa kuzingatia muda. “Kuswali ni muhimu, wahamasisheni waumini kushiriki katika ibada.”

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwasihi waumini hao wawazoeshe watoto wao kufanya ibada ili wawe watoto wema. Pia aliwasihi viongozi wa msikiti huo waimarishe kitengo cha elimu na watumie nyumba za ibada kupata mawaidha mbalimbali.

Awali, Imamu wa msikiti wa Msalato, Sheikh Aboubakar Abdallah Omar alitumia fursa hiyo kuwasisitiza waumuni juu ya umuhimu kuishi kwa unyenyekevu na kumtegemea Mwenyezi Mungu katika maisha yao na wajiepushe na vitendo vya ufisadi.

No comments: