RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI MISA YA DOMINIKA YA 32 MWAKA A KATIKA PAROKIA YA BIKIRA MARIA IMAKULATA CHAMWINO IKULU DODOMA LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu-Chamwino Mkoani Dodoma kwa kuanzisha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Chamwino ambao umekamilika na kuanza kutumika.
Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli ametoa shukrani hizo katika Misa Takatifu ya Jumapili ya 32 ya Mwaka “A” iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Paul Mapalala.
Amewashukuru Waumini wa Madhehebu mengine ya Dini waliojitokeza kuchangia ujenzi wa Msikiti huo pamoja na Kanisa la Bikira Maria Imakulata Ikulu-Chamwino ambalo ujenzi wake ulifanyika kabla, na amebainisha kuwa kitendo hicho kinadhihirisha umoja, upendo na mshikamano wa dhati walionao Watanzania.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ambaye leo amesali Ibada ya kwanza ya Jumapili tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili amewashukuru Waumini wa Madhehebu yote ya Dini kwa Sala na Dua zao za kuombea mchakato wa uchaguzi mkuu tangu wakati wa kampeni hadi kuapishwa kwake na amesisitiza kuwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais ni ushindi wa Watanzania wote.
Amewaomba viongozi wa Dini na Watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa, na kuiombea Serikali anayoiongoza ili itekeleze ahadi zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020/25 zilizolenga kujenga uchumi imara na ustawi wa jamii.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
08 Novemba, 2020
Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea Sakramenti Takatifu toka kwa Padre Paul Mapalala waliposhiriki Misa ya Dominika ya 32 Mwaka “A” katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu Dodoma leo Jumapili Novemba 8, 2020. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru baada ya kupokea Sakramenti Takatifu toka kwa Padre Paul Mapalala wakati wa Misa ya Dominika ya 32 Mwaka “A” katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu Dodoma leo Jumapili Novemba 8, 2020. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia waumini wenzie baada ya kupokea Sakramenti Takatifu toka kwa Padre Paul Mapalala wakati wa Misa ya Dominika ya 32 Mwaka “A” katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu Dodoma leo Jumapili Novemba 8, 2020.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe wakiondoka kanisani baada ya Misa ya Dominika ya 32 Mwaka “A” katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu Dodoma leo Jumapili Novemba 8, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika
Misa ya Dominika ya 32 Mwaka “A” katika Parokia ya Bikira Maria
Imakulata Chamwino Ikulu Dodoma leo Jumapili Novemba 8, 2020
PICHA NA IKULU
No comments: