RAIA WIWILI WA KIGENI WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 30 KWA KUKUTWA NA HATIA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA AINA YA HEROINE.
Na Karama Kenyunko globu ya jamii
RAIA wawili wa Iran Nabibaksh Pribaksh Bidae nahodha wa Jahazi na Injinia wake, Muhamad Hanif wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilogramu 111.02
Hukumu hiyo ya kesi ya uhujumu uchumi namba 14/2018 dhidi ya bidae na wenzake 12, imesomwa Novemba 6, 2020 na Jaji Imakulata Banzi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi baada ya washtakiwa hao kutiwa hatiani
Aidha Mahakama Kuu pia imeamuru jahazi lililohusika kusafirisha dawa hizo za kulevya litaifishwe na dawa husika ziteketezwa.
Hata hivyo mahakama hiyo imewaachiwa washtakiwa 11waliokuwa washtakiwa pamoja nao baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo
Washtakiwa walioachiwa huru Abdallah Sahib, UIbeidulla Abdi, Naim Ishaqa, Moslem Golmohamad, Rashid Badfar, Omary Ayoub, Tahir Mubarak and Abdulmajid Pirmuhamad, ambao wote ni raia wa Iran pamoja na watanzania wawili, Ally Abdallah na Juma Amour.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Banzi amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wao 10 waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa watu hao wawili walitenda kosa hilo
Hata hivyo, mapema kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, Jaji Banzi aliuza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ndipo wakili wa Serikali Monica Mbogo aliyekuwa akisaidiana na Cecilia Sheli aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao na kwa wengine walio na mpango wa kufanya makosa kama hayo.
Katika kesi washtakiwa walikuwa wakitetewa na Mawakili wa Utetezi Juma Nassoro na Jethro Tiliemwesiga.
Nabibaksh Pribakish Bibade na wenzake 12 walikamatwa tarehe 24, mwezi 10, 2017 majira ya saa nne na robo usiku katika bahari ya Hindi na Maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wakishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
No comments: