Njombe:Wakurugenzi,wakuu wa wilaya waagizwa kusimamia utoaji chanjo za HPV


 Na Amri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mhandisi Marwa Rubirya ameagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi mkoani humo kusimamia na kufuatilia hatua za kuhakikisha wasichana wenye umri wa chini ya miaka 14 wanapata dozi mbili na tatu za HPV ya chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi.

Akifungua kikao cha kujadili mikakati ya kuinua kiwango cha dozi ya pili ya saratani ya mlango wa kizazi katika mkoa wa Njombe mpango unaoratibiwa na Shirika la Jhpiego, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Marwa Rubirya amesema amebaini kuna makundi matatu ya vijana wakiwemo walioathirika na maambukizi ya VVU hawajapata chanjo hiyo..

"Vile vile hawa wasichana ambao wana maambukizi ya virusi vya ukimwi nao ni muhimu wakashirikishwa katika zoezi hili la kupata chanjo,na wao tumejifunza wanatakiwa kupata chanjo tatu"alisema Rubirya

Aidha Rubirya amesema mkoa unaowajibu wa kujifunza mafanikio yaliyopatikana kutoka mikoa mingine.

"Tumejifunza kutoka kwa wenzetu waringa sasa tuje na mikakati ambayo itatusaidia kuhakikisha tunaendeleza mafanikio amabyo tutayapata mwishoni mwa programu hii"alisema tena Marwa

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Bumi Mwamasage pamoja na mratibu wa Afya ya uzazi na mtoto, Felisia Hyera na Dk. Maryrose Giattas ambaye ni mratibu wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kutoka shirika la Jhpiego wamesema ni muhimu kupata chanjo ya HPV ili kuokoa maisha ya wasichana na wanawake hivi sasa..

"Chanjo hii inalenga kuzuia saratani kwa kundi hilo kwani kina mama ndio wanao patwa na shida hiyo wanapofikia umri uliozidi miaka 30 "alisema Dk. Bumi Mwamasage

Kikao hicho kilichowashirikisha wajumbe kutoka Taasisi za Dini, Jeshi la Polisi pamoja na uwakilishi wa wanawake michango mbalimbali kuhusu namna ya kuwezesha kampeni hiyo ilitolewa.

"Jeshi la polisi nalo lina nafasi kubwa kuhakikisha watoto wanakuwa salama,na katika kuchukua hatua kwa wale wanaowafanya watoto wasiweze kupata chanjo"alisema alisema Kamanda Hamis Issa 

Mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya wakati akizungumza na wajumbe waliofika katika kikao cha kujadili mikakati ya kuinua kiwango cha dozi ya pili ya saratani ya mlango wa kizazi katika mkoa wa Njombe.
 Baadhi ya wajumbe wakiwa makini kusikiliza wataalamu wakati wa kikao cha  cha kujadili mikakati ya kuinua kiwango cha dozi ya pili ya saratani ya mlango wa kizazi katika mkoa wa Njombe.

No comments: