Njombe:Wakulima wa parachichi waomba kushushiwa ghalama za pemebejeo

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wakulima wa zao la parachichi mkoani Njombe wanaiomba serikali kuboresha ghalama za pembejeo hususani zinazotumika katika kilimo hicho,ili kuwasaidia wakulima na kunufaika na kilimo hicho ambacho kinaendelea kukuwa kukua kwa kasi katika maeneo ya mkoa wa Njombe.

Elijius Wela ni mkulima wa parachichi na mkurugezni wa kampuni ya MADEBE inayoshughulika na upandaji wa parachichi kutoka kwenye kitalu kwenda shambani,akizungumza na vyombo vya habari shambani kwake amesema wakulima wengi kwao changamoto ni ghalama ya Pembejeo,wanaomba serikali kushusha bei ya Pembejeo pamoja na kuweka ruzuku ya kutosha ili zao hili liendelee kukua na kukuza zaidi uchumi wa Njombe na taifa kwa ujumla.

"Serikali ikazane kuangalia pembejeo za zao la parachichi iwe chini na waweke ruzuku ya kutosha ili kuleta unaafuu kwa wakulima"alisema Wela.

Amesema wananchi wamehamasika kuingia katika zao hilo kutokana uzuri kibiashara na kuwasadia wengi kufanikiwa kiuchumi.

"Kwa kweli parachichi inalipa kwasababu mkulima akifanikiwa kupanda shamba Ekari moja na miti ikitimiza mika 7 na kuhudumia vizuri hawezi kukosa milioni ishirini na atafanikiwa sana na tunashukuru serikali inavyotuuunga mkono kwa kuwa inatupatia zao ambalo lipo soko kidunia,na tuna uwezo Zao hilo litatupeleka mbali mkoa wa Njombe Kiuchumi"Aliongeza Wella

Baraka Muyamba na Jiskaka Mwalyego ni baadhi ya watumishi wanaofanya kazi katika kitalu cha uzalishaji wa parachichi kilichopo kijiji cha Kifanya halmashauri ya mji wa Njombe kinachomilikiwa na bwana MADEBE,wanasema licha ya kufanya kazi katika kampuni hiyo lakini  wamehamasika kuingia katika kilimo kutokana faida inayotokana na zao hilo.

"Kwanza kampuni hii imekuwa msaada mkubwa kwa kupata ajira inayotusaidia kukidhi mahitaji,na mimi nimehamasika kwenye kilimo hiki lakini bado tunaendeleea kupata elimu zaidi ili tuweze kunufaika"Alisema Baraka Muyamba

"Mimi nipo nafanya kazi hapa ya Grafting,na kwa kweli kwa mkoa wa Njombe parachichi linakubali na lina faida na kwa kuhamasika kwangu tayari Mbeya nina shamba Ekari 60 amabyo yanaandaliwa na mengine ni mapori kwa ajiri ya kwenda kuanza kilimo cha Parachichi"alisema Jiskaka Mwalyego

Sadam Fundikila ni meneja wa kampuni ya MAKE A FOREST DEVELOP BEST COMPANY LTD (MADEBE) amesema kampuni hiyo inayohusika na utoaji wa huduma mbali mbali za kilimo hususani Parachichi,wamekuwa na msaada kwa jamii hususani kijiji cha Kifanya kwa kufanikiwa kuajili vijana 200 wanaolipwa kwa kazi na 5 wakilipwa kwa mwezi huku pia wakiendelea kutafuta masoko ya zao la parachichi kwa wakulima.

"Lakini pia tumeanzisha mpango wa kuwa na kikundi kwa wakulima kitakachojihusiha na uzalishaji wa parachcichi,licha ya kuendelea kuhusika na utoaji wa huduma za kilimo kwenye mazao ya misitu na matunda kwa maana ya parachichi"alisema bwana Fundikila

Mmoja wa mtumishi akiendelea na zoezi la umwagiliaji wa miche ya parachichi
Jiskaka Mwalyego akiendelea na zoezi la Grafting katika kitalu cha miche ya Parachichi ya bwana MADEBE mjini Njombe.

Eneo la Kitalu cha miche ya parachichi iliyostawi inayomilikwa kampuni ya MADEBE eneo la kifanya halmashauri ya mji wa Njombe ikionekana baada ya kupigwa picha
Elijius Wela ni mkulima wa parachichi na mkurugezni wa kampuni ya MADEBE,akifafanua namna zao la parachichi linavyowanufaisha wananchi wa Njombe huku akiomba wakulima wa zao hili kuendelea kulima kwa kufuata taratibu ili kufanikiwa kiuchumi kuptia zao hilo.
Sadam Fundikila meneja wa kampuni ya MAKE A FOREST DEVELOP BEST COMPANY LTD (MADEBE) akieleza namna kampuni hiyo inavyofanya shughuli zake kwa wakulima pamoja kusaidia utojai wa elimu.

No comments: