NAMUNGO FC YAGAW NAMUNGO FC YAGAWA KOROSHO KWA WASUDAN A KOROSHO KWA WASUDAN

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Klabu ya Soka ya Namungo ya Wilayani Ruangwa mkoani Lindi imeanza vyema Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CONFEDERATION CUP) baada ya kupata ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Al-Rabata FC ya Sudan Kusini katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.

Namungo FC ilianza kugawa Korosho hizo katika dakika ya 19 kupitia Kwa Mshambuliaji wake, Raia wa Ghana, Stephen Sey baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Beki ya Kushoto, Edward Charles Manyama. Bao lilifungwa na huyo huyo, Sey dakika ya 39 akizungusha mpira safi ulimshinda mlinda lango wa Al-Rabata FC.

Msumari wa mwisho na wa tatu ulididimizwa na Mshambuliaji machachari, Shiza Ramadhan Kichuya dakika ya 63 aliyeingia kipindi cha pili cha mchezo huo kuchukua nafasi ya Mshambuliaji Bigirimana Blaise.

Kwa matokeo hayo, Namungo FC inajiweka katika nafasi nzuri ya kusongo mbele katika Michuano hiyo wakati ikisubiri mchezo wa marudiano wiki baadae nchini Sudan Kusini kati ya Desemba 4 na 6, 2020.

No comments: