MWINJILISTI ROBERTS WA CFAN AKUNWA NA JUHUDI ZA TANZANIA ZILIZOSAIDIA KUSHINDA COVID -19

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Injili mkoani
Tabora Askofu Peter Shani akizungumza na waandishi wa habari jana
kuhusu mkutano huo utakaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 15 Mwezi huu
mjini humo.
Mwinjilisti na Mkurugenzi wa maandalizi ya  Mkutano mkubwa wa
Injili Randy Roberts( wa pili kutoka kulia) akizungumza jana  na
waandishi wa habari mjini Tabora kuhusu mkutano huo utakaofanyika
kuanzia tarehe 12 hadi 15 mwezi huu mjini humo.


Na Tiganya Vincent, Tabora

WATANZANIA wamepomgezwa kwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID -19)  ambapo wameweza kuushinda na kuufanya utoweke nchini humo.

Kauli hiyo imetolewa  na Mwinjilisti na Mkurugenzi wa maandalizi ya
 Mkutano mkubwa wa Injili Randy Roberts wakati wa mkutano na waandishi
wa habari mjini Tabora.

Amesema Watanzania wakiongoizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli wamefanikiwa kuondoa tatizo
hilo na kuwawezesha kuendelea na shughuli mbalimbali.

“Watanzania hawakukubali kuupigia magoti ugonjwa wa COVID 19 badala
yake walimuinua Mungu juu na hatimaye wamefanikiwa kuushinda …hongreni sana.” amesema.

Amesema hali hiyo imewawezesha kuendelea kwa  shughuli zinawaunganisha
watu pamoja ikiwemo mikutano ya Injili na shughuli nyingine za Ibada.

Roberts amesema kutokana na uwepo wa mazingira salama nchini Tanzania
wanatarajia kuendesha Mkutano Mkubwa wa Injili mkoani Tabora kuanzia
wiki ijayo kwa ajili ya kuendelea kuwaombea watu wenye matatizo
mbalimbali.

Mkurugenzi huyo amesema katika baadhi ya Nchi za jirani na Tanzania
wameshindwa kuendesha mikutano ya Injili kutokana na kuendelea kuwepo
kwa  ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID -19)

Ameeleza kuwa, ndani ya wiki mbili zijazo wanatarajia kuwa na mikutano ya
Injili katika maeneo ya Singida , Arusha, Shinyanga, Tabora na Kahama
ambapo Mwinjilisti Jared Horthon ataongoza katika kuwaombea wakazi wa
maeneo hayo.

No comments: