MWENYEKITI WA TUME YA MADINI AKUTANA NA KAMPUNI YA AGA BULLION
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amekutana na kampuni inayojihusisha na utafiti, uchimbaji, usafishaji na biashara ya dhahabu kutoka Uturuki ya AGA BULLION katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Madini zilizopo jijini Dodoma.
Walioshiriki katika kikao hicho walikuwa ni pamoja na Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya na Meneja wa Biashara ya Madini, George Kaseza.
Akizungumza katika kikao hicho Profesa Kikula amesema kuwa, lengo la ziara ya kampuni ya AGA BULLION kwenye ofisi za Tume ya Madini ni kujifunza biashara ya madini nchini na majukumu ya Tume ya Madini hususan katika eneo la utoaji wa leseni za madini na biashara ya madini.
Katika hatua nyingine, Profesa Kikula ameikaribisha kampuni hiyo kuwekeza kwenye Sekta ya Madini kwa kushirikiana na Taasisi za Serikali lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu kwenye teknolojia ya utafiti, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini.
No comments: