Mrembo wa utalii Tanzania atembelea Njombe,waweka mkakati kutembelea vivutio
Zawadi Mwambi mwakilishi wa mkoa wa Njombe katika shindano la mrembo wa utalii Tanzania akizungumza jambo na wataalamu kutoka ofisi za mkuu wa mkoa wa Njombe mara baada ya kukamilisha mazungumzo ofisini hapo
Zawadi Mwambi mwakilishi wa mkoa wa Njombe katika shindano la mrembo wa utalii Tanzania akizungumza na Katibu Msaidizi Uchumi na Uzalishaji katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe, Ayoub Mndeme alipofika ofisini kwake.
Zawadi Mwambi mwakilishi wa mkoa wa Njombe katika shindano la mrembo wa utalii Tanzania akizungumza mara baada ya kuwasili katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Njombe.
======= ======= ============
Wananchi mkoani Njombe wameshauriwa kuenzi na kuvitembelea vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya maeneo yanayowazunguka kwa lengo la kufahamu vyema rasilimali za taifa zilizopo Nyanda za Juu Kusini.
Rai hiyo imetolewa na mwakilishi wa mkoa wa Njombe katika shindano la mrembo wa utalii Tanzania, Zawadi Mwambi wakati alipotembelea ofisi za mkuu wa mkoa wa Njombe kwa ajili ya kujitambulisha na kupata ushirikiano wa kuihamasisha jamii mkoani hapa na kutumia wasaa wa kuvitembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Nyanda za Juu Kusini ili kujifunza ..
"Leo nimefika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe kufanya mazungumzo ya kuangalia jinsi gani tunaweza kufanya ili kukuza vivutio vinavyopatikana katika mkoa wetu na kutoa elimu kwa jamii lakini zaidi mashuleni kwa wanafunzi waweze kutambua na kutembelea na wakipata elimu katika mashule naimani wataendelea kukua na ile elimu"alisema Zawadi Mwambi
Baadhi ya wadau wa sekta ya utalii Nyanda za Juu Kusini akiwemo Michael Karam ameshauri kuwepo na hamasa ya serikali ya mkoa kuvumbua vivutio vipya vilivyopo..
"Ni lazima pia kuwepo utaratibu wa kuvumbua vivutio vipya ili wageni wa ndani na wa Nje waeze kuvijua na kuto kuvizoea vile walivyovizoea vya kila siku"alisema Michael Karam
Naye Katibu Msaidizi Uchumi na Uzalishaji katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe, Ayoub Mndeme amemshukuru mwakilishi wa mkoa wa Njombe katika mashindano ya urembo wa utalii na kuahidi mkoa kumpa ushirikiano katika kutangaza vivutio vya utalii mkoa wa Njombe.
"Kwa keli fursa za utalii zinahitaji kufahamika kuanzia kwa wanafunzi kama alivyozungumzia kwasababu haya ni maeneo ambayo sisi tupo na tunaishi na utalii imbao unahamasishwa sasa hivi ni ule wa ndani "alisema , Ayoub Mndeme
No comments: