MRADI WA MAJARIBIO WA DAWA WAZINDULIWA
*Mganga Mkuu wa Serikali ataka gharama kwa wanafunzi watafiti zipungwe
*TMDA kutoa mafunzo kwa wadau kujenga uelewa
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa itatoa ushirikiano katika mradi wa Ascend unaolenga kuboresha mifumo ya udhibiti wa majaribio ya dawa,tafiti mbalimbali na udhibiti wa usalama wa dawa zitakazoleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Hayo ameyasema Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Abel Makubi wakati akizundua Mradi wa miaka miwili wa uboreshaji wa mifumo ya Udhibiti wa majaribio ya dawa ambao uko chini ya Mamlaka ya Dawa ,Vifaa Tiba (TMDA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Dkt. Makubi amesema katika uzinduzi wa mradi wa ASCEND unaolenga kuimarisha Tafiti za majaribio ya dawa pamoja na maadili ya tafiti za afya nchini na kufuatilia usalama wa madhara yatokanayo na matimizi ya dawa hayo.
Mradi huo ni unalenga kupunguza muda wa kutathmini maombi ya kufanya tafiti za majaribio ya dawa nchini na kuwezesha upatikanaji wa vibali vya utafiti kwa muda mfupi.
Taasisi zinazoshiriki katika mradi ni Mamlaka ya Dawa,Vifaa Tiba (TMDA), Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR,) Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar(ZFDA,) KCRI, MUHAS, ZAHRI na ST. Andrew's University ya Uingereza pia mradi huo ambao ni wa miezi 30 utasaidia kujengea uwezo watafiti wachanga kwa kupata mafunzo mbalimbali toka MUHAS na kuimarisha mifumo ya tafiti mbalimbali za Afya nchini.
Dkt. Makubi ameiangiza TMDA kupunguza gharama kwa wanafunzi wanaofanya Utafiti kwani wao ndio wanaotegemewa kuwa wataalam kuja kuhudumia taifa.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa ,Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo amesema katika Mradi huo pia watatoa mafunzo katika Kituo cha Muhimbili ili kujenga uelewa mpana kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Amesema kuwa kupatikana kwa mradi huo wamepitia miongozo mbalimbali na kusaidia TMDA kupata ruzuku hizo katika mradi.
"Mradi huu utaleta matokeo chanya katika masuala ya majaribio ya tafiti za dawa na hivyo Taifa kunufaika katika maendeleo ya tafiti hizo ambapo nchi zingine zilishapata na zikaweza kupata mafanikio."amesema Fimbo.
No comments: