MIAKA 40 YA NIMR, WAFANYAKAZI WAJIVUNIA KUPUNGUZA VIFO VYA BINADAMU KUPITIA TAFITI
TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), yaandimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake huku wakijivunia kufanya tafiti zinazo kuboresha matibabu kwa wagonjwa wenye vimelea vya Malaria, kupunguza magonjwa na vifo hapa nchini.
Hata hivyo wafanyakazi wa Taasisi hiyo wajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo 1980 hadi sasa 2020.
Akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka 40 ya NIMR, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Yunus Mgaya amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwani ilianza kwa kuwa na kituo kimoja 1980 na sasa ina vituo vikubwa saba na vituo vidogo saba katika mikoa nane hapa nchini.
Akizungumzia kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika tafiti kwa miaka hiyo 40 Mgaya amesema kuwa NIMR imechangia katika uboreshaji wa uchunguzi na matibabu ya virusi ya UKIMWI (VVU).
Hata hivyo amesema kuwa NIMR imetoa mchango mkubwa katika utekelezaji w sera na mapambano dhidi ha Malaria katika utafiti uliofanywa katika vituo vya NIMR Amani na NIMR Tanga ambapo walichangia katika mabadiliko ya tiba ya Malaria kutoka dawa ya SP hadi dawa ya Mseto.
"Tafiti hizi zimesababisha kuboresha matibabu kwa wagonjwa wenye vimelea vya Malaria na mwishowe kupunguza magonjwa na vifo hapa nchini." Amesema Mgaya.
Licha ya hayo amesema kuwa tafiti zilizofanywa na NIMR zimeleta matokeo ambayo yametumiwa na shirika la afya duniani (WHO) katika kuboresha miongozo yake katika tiba ya malaria.
Amesema kuwa mapema 1990 kituo cha amani kilitafiti matumizi ya vyandarua vyenye viwatilifu na matokeo ya utafiti huo yalisababisha kupitishwa kwa matumizi ya vyandarua vyenye dawa ikiwa ni mkakati wa kudhibiti malaria.
Mgaya amesema kuwa NIMR Muhimbili wakishirikiana na Mpango wa taifa wa kudhibiti Kifua kikuu (TB) waliweza kuinua kiwango cha ubora wa utoaji huduma katika uchunguzi wa vimelea vya Kifua Kikuu (TB) katika maabara kuu na kufikia viwango vya kimataifa.
Mgaya amesema katika kipindi cha Mlipuko wa ugonjwa wa Corona hapa nchini NIMR kupitia idara ya Utafiti wa Tiba ya Asili ya Mabibo iliandaa matibabu ya mitishamba au miti dawa na tiba mbadala ambazo kwa sasa zinafanyiwa utafiti ili kupima ufanisi wake ikiwa dawa hizo ni pamoja na NIMRCAF na kinywaji chenye vitamini na lishe cha NIMREVIT, dawa ya pamoja nadawa ya PERSIVIN ambayo inatibu uvimbe wa tezi dume, NIMREGINEN ambayo ni dawa ya matibabu ya saratani, MUNDEX inayoongeza nguvu za kiume.
Kuhusu Magonjwa yasiyoambukiza Mgaya amesema kuwa magonjwa hayo yamekuwa tishio kubwa kwa afya ulimwenguni hivyo katika kisheherekea miaka 40 ya NIMR wameanza kufanya maonesho katika maeneo mbalimbali kwaajili ya wananchi kupima bila gharama yeyeto na kutoa elimu juu ya kuepukana na magonjwa hayo.
"NIMR nimetoa mchango mkubwa katika kutekeleza sera za kudhibiti ugonjwa wa Usubi, Malale, kichocho matende na mabusha.
Katika miaka 40 ya NIMR imejipanga kwa Novemba na Desemba 2020 kufanya maonesho katika vituo vyote Vikubwa vya NIMR na makao Makuu kwa kuonesh shughuli za kitafiti zinavyofanya, kutoa huduma wezeshi, kuchangia damu na uchunguzi wa magonjwa mbalimbali hasa yasiyo ambukiza kama vile kisukari, saratani, macho na shinikizo la damu.
Vituo vitakavyokuwa na maonesho ya NIMR ni Amani, Mwanza, Muhimbili, Tabora, Tanga, Mbeya na Dodoma.
No comments: