MGANGA MKUU WA SERIKALI AWAPONGEZA JKCI NA MOI KWA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Makubi akiwajulia hali wagonjwa waliofika kupata huduma kwenye Taasisi ya MOI
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimuonesha Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ukarabati unaoendelea kwenye taasisi hiyo kwa mapato ya ndani
Wodi ya Watoto iliyopo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) ambayo ukarabati wake unakamilika hivi karibuniMenejimenti ya Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu(MOI) wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Serikali(hayupo pichani) wakati alipofika hospitalini hapo kujionea hali ya utoaji huduma za afya
***********************************
Na.WAMJW-Dar es Salaam
Mgaga Mkuu wa Serikali Prof.Abel Makubi leo amefanya ziara ya kikazi kwenye taasisi ya JKCI na MOI na kujionea hali ya utoaji huduma katika hospitali hizo
Pof. Makubi amewashukuru na kuwapongeza Uongozi na watumishi wa taasisi hizo mbili kwa kazi kubwa wanazofanya katika kuwahudumia wananchi na kuwataka wafanye kazi kwa bidii na kwa uzalendo hususan kuwahudumia wananchi wasio na uwezo.
Vilevile amewataka kuendeleza mshikamano katika kuboresha huduma ili wananchi waweze kupata huduma nzuri na bora.
Kwa upande wa JKCI,Mganga Mkuu huyo aliwapongeza kwa kutumia mapato yao ya ndani kuboresha huduma kwenye hospitali hiyo
Hata hivyo amewataka MOI kutoa wataalam wake kwenda kutoa huduma na ujuzi kwenye hospitali za kanda ili huduma za mifupa na mishipa ya fahamu isifuatwe Dar es Salaam pekee
No comments: