MDAU WA ELIMU KAYUNI AKABIDHI KOMPUTA SHULE YA SEKONDARI UKWAAMANI
Mdau wa Elimu na Maendeleo David Kayuni akizungumza na wanafunzi na Walimu wa Shule ya Sekondari Ukwamani alipokwenda kutoa msaada wa komputa katika shule hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukwamani Saphina Egha akizungumza kuhusiana namna walivyopokea msaada wa komputa.
Mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ukwamani Khadija Selemani akitoa shukurani kwa wanafunzi wenzake mara baada ya kukabidhiwa komputa katika shule hiyo.
******************
Na Amir Atick, Michuzi Tv Mdau wa elimu na Maendeleo David Kayuni amekabidhi komputa Tano (5) katika shule ya Sekondari Ukwamani-Kawe Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam zenye thamani ya Sh.3.2.
Akizungumza Mara baada ya kukabidhi komputa hizo Kayuni amesema kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inakuwa kwa kasi hivyo wanafunzi wanatakiwa kujua Teknolojia mapema kabla hawajafika hawajafika katika elimu ya juu.
Amesema kuwa wanafunzi wa Sekondari wakipata mwanga wa Tehama wakati wakiwa Sekondari watakuwa wanafunzi wenye uwezo katika elimu ya Sekondari na vyuo.
"Ninaamini komputa hizi mtazituza ikiwa ni pamoja na kuzitumia katika masomo na mtumie kwa usalama zaidi kwani msipotumia kwa usalama zinaweza kuwapotosha hasa katika masuala ya wa data 'Internet'"amesema Kayuni.
Aidha amesema kuwa licha ya kutoa komputa hizo ataendelea kuwa na ukaribu wa shule hiyo katika kusukama gurudumu la elimu kwenda mbele zaidi na kuongeza kuwa nchi imeingia katika uchumi wa kati hivyo kunahitaji kuwa na wataalam wa kuweza kwenda na uchumi huo.
Amesema serikali imewekwa mikakati ya kuboresha elimu hivyo Kama wadau hatutakiwi kuwa nyuma katika kwenda na serikali kwa kuunga mkono.
Nae Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukwamani Mkuu wa shule Saphina Egha amesema anawakaribisha wadau wengine wa elimu na maendeleo kuleta misaada mbalimbali itakayo wanafunzi katika kujifunza na kutimiza ndoto zao hapo mbeleni.
Amesema kuwa komputa kwa sasa zinahitajika kwani dunia inatoka katika mfumo wa karatasi na kuingia kutumia komputa.

No comments: