MBUNGE KAMONGA AWASHUKURU WANALUDEWA BAADA YA KUAPISHWA.


Na Shukrani Kawogo, Dodoma.

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amewashukuru wote waliokuwa sambamba nae katika mchakato mpaka kufikia kuwa  mbunge kwani wamempa ushirikiano mzuri.

Hayo ameyasema katika sherehe baada ya kuapishwa aliyoifanya na baadhi ya wanaludewa pamoja na watu mbalimbali walioalikwa kushiriki sherehe hiyo.

Alisema Wana Ludewa wameonyesha Imani kubwa kwake mpaka kumpa nafasi hiyo ya uongozi hivyo anaahidi kuwatumikia vyema na kuleta Maendeleo katika jimbo hilo.

Aidha kwa upande wa wakazi hao wa Ludewa wamesema wameamua kuja Dodoma kumsapoti mbunge wao kwani wanajua atakuwa chanzo Cha maendeleo na kuwa mbunge wa kudumu.

Mbunge huyo aliapishwa oktoba 10  majira ya saa 11 jioni ambapo baada ya kuapishwa wananchi pamoja na ndugu walimpokea kwa shangwe nyingi.

Na baada ya shughuli za kibunge kumalizika wananchi waliunga na mbunge wao kufanya sherehe katika ukumbi wa Royal village uliopo jijini Dodoma.
 

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (Mwenye suti nyeusi) akishangiliwa na baadhi ya ndugu na jamaa nje ya ukumbi wa bunge baada ya kutoka kuapishwa 

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa ukumbi katika sherehe ya kumpongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga baada ya kuapishwa katika ukumbi wa Royal village uliopo jijini Dodoma.

Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume (kushoto) akimtambulisha  mwenyekiti wake wa chama hicho wa wilaya hiyo  Stanley Kolimba kwa wageni waalikwa(hawapo pichani) katika sherehe ya kumpongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga katika ukumbi wa Loyal village jijini Dodoma.

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama  wa CCM na wadau mbalimbali nyumbani kwake jijini Dodoma ambao walikuja kimsindikiza kwenda kuapishwa.

Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM wilaya ya Ludewa Theopista Mhagama (wakwanza kushoto) akiongea na wageni waalikwa (hawapo pichani) anayefuata ni mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga na katibu wa CCM wilaya Bakari Mfaume.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa na baadhi ya ndugu zake nje ya  ukumbi wa bunge. Kushoto kwake ni mke wake, kulia ni mama yake mzazi anayefuata ni dada yake na nyuma yake ni wadogo zake pamoja na dada yake.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akimlisha keki mke wake wakati wa sherehe ya kumpongeza mbunge huyo baada ya kuapishwa iliyofanyika katika ukumbi wa Loyal village jijini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa na mkewe wakikata keki katika sherehe ya kumpongeza mbunge huyo iliyofanyika katika ukumbi wa Loyal village uliopo jijini Dodoma.

No comments: