Magonjwa yasiyoambukiza yanakua kwa kasi-Kunenge

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Abubakar Kunenge akizungumza katika kilele cha Maadhimisho Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Grace Maghembe akizungumza namna walioendesha Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza katika kutoa elimu pamoja na upimaji wa afya.
Mwenyekiti wa Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Profesa Andrew Swai akitoa maelezo ya Ugonjwa wa Kisukari.
Afisa wa Uanchama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Ganeth Haule akiwahudumia wananchi walipotembelea Banda la NHIF katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yaliyokuwa yalifanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Thomas Mkusa akiwapa maelezo wananchi umuhimu wa Bima ya Afya.
Wananchi wakiwa katika foleni kwa ajili ya kupata vipimo katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza ndani ya viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


*Ugonjwa wa Kisukari watajwa kuchukua asilimia 11 ya Bajeti yote ya Afya Duniani

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.
Imeelezwa kuwa magonjwa yasiyoambukiza yanachangia vifo milioni 41 ambayo no sawa na asilimia 72 ya vifo vyote milioni 47 vilivyotokea mwaka 2018  kwa mujibu wa  Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka 2018.

Wakati huo huo taarifa za mwaka 2013 za Shirika la Maendeleo (UNDP) zinaonyesha kuwa pamoja na changamoto za kiafya ya Magonjwa yasiyoambukiza yanaathiri Sana nyanja zingine za maisha n jamii kwa ujumla na kubashiriwa kuwa kufikia mwaka 2033 gharama zitokanazo  na huduma kwa wagonjwa hayo yatafikia Dola za Kiamrekani Trioni 47 ambapo fedha hizo zilitakiwa kutumika kupunguza umasikini kwa watu Bilioni 2.5 kwa miaka 50.

Hayo aliyasema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge katika kilele cha Maadhimisho Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika kwa wiki nzima kwa Hospitali na Taasisi zinazojighulisha na Afya kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kunenge amesema kwa nchi za uchumi wa kati na chini Magonjwa yasiyoambukiza yatagharimu mataifa hayo jumla ya Dola za Kimarekani Trioni 7 kwenye kipindi cha 2011 -2025.

Aidha amesema makadirio yanaonyesha kuwa gharama za huduma ya Magonjwa yasiyoambukiza itafikia asilimia 75 ya mzigo wore wa bajeti ya afya Duniani huku Ugonjwa wa Kisukari pekee ulikipeleka gharama za Dola za Kimarekani Bilioni 465 sawa na asilimia 11 ya bajeti ya Afya duniani.
Amesema kuwa takwimu za kitaifa ya hali ya Magonjwa yasiyoambukiza pia inaonyesha kuwa tatizo hili lipo nchini na linaongezeka kwa kasi  na ongezeko lake ni asilimia 24 ndani ya miaka miwili hivyo ni kubwa Sana linahitaji mikakati madhubuti kukabiliana na Magonjwa hayo.

Kunenge amesema kunahitaji ushirikiano wa kuongeza nguvu katika mapambano ya kuweza kufikia malengo ya kukinga na Kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza kwa kuzuia na Kudhibiti matumizi ya vilevi vikiwemo sigara na Pombe ,Kuhamasisha watu kufanya mazoezi au shughuli za nguvu ,Sukari pamoja na mafuta.

Nae Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Grace Maghembe amesema katika Maadhimisho hayo wamefanya vipindi mbalimbali katika vyombo vya Habari vipatavyo 30 ikiwa ni kuelimisha wananchi.

Dkt.Maghembe amesema wamewafikia wanafunzi 1000 kwa shule 50 za Msingi na Sekondari  huku matangazo yakiwa zaidi ya 40 machapisho 200 pamoja na kungamano la kisayansi kwa wataalam wa afya 500 walishiriki.
Nae Mwenyekiti wa Chama Wagonjwa Kisukari Profesa Andrew Swai amesema watu warudi katika kwa kuepuka vitu vilivyokubolewa.

Amesema magonjwa hayo zamani hayakuwepo lakini sasa yapo hiyo inatokana na kuacha asili.

No comments: