MAELFU YA WANANCHI, WAGENI WAALIKWA WASHUHUDIA DK.MAGUFULI AKIAPISHWA



Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Dodoma

RAIS Dk.John Magufuli ameapishwa leo jijini Dodoma mbele ya maelfu ya wananchi wa Watanzania pamoja na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali wakiwemo marais,makamu wa Rais , mawaziri na viongozi wa dini.

Kabla ya kula kiapo, Dk.Magufuli aliingia Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma saa nne asubuhi na kisha kuzunguka uwanja kwa ajili ya kusalimia maelfu ya wananchi akiwa katika gari ya wazi. Baada ya kuzunguka uwanja alishuka kwenye gari na kisha kuelekea eneo maalum kwa ajili ya wimbo wa Taifa sambamba na mizinga 21.Baada ya hapo ikashushwa bendera ya Rais ikiwa ni ishara ya kuhitimisha awamu ya kwanza ya uongozi wake

Hata hivyo baada ya kushushwa bendera ya Rais alielekea jukwaa maalum kwa ajili ya kwenda kula kiako ambapo Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ndiye alimuapisha na kisha alipewa ngao na wazee wawili mmoja kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka Tanzania Visiwani.Baada ya hapo alienda kukaa kitini.

Akiwa amekaa ikafuata hatua ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kula kiapo cha kutumikia nafasi hiyo.Walipomaliza kula kiapo ikafuata nafasi ya dua ambayo iliombwa na viongozi wa dini zote.

Baada ya dua hiyo kumalizika Rais Dk.Magufuli, Makamu wa Rais akiwa ameongozana na Jaji Mkuu, wazee, viongozi wa dini,Mwanasheri Mkuu walifanya maandamano wakitoka jukwaaa ambalo lilitumika kwa ajili ya kumuapisha.Wakati huo gwaride lilikuwa limetengeneza umbo la Alfa kuashiria kuanza kwa muhula wa pili wa miaka mitano ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Wakati tukio hilo likiendelea utulivu uwanjani hapo ulikuwa mkubwa, wananchi na wageni waalikwa walikuwa kimya, Rais Magufuli alienda eneo maalun kwa ajili ya gwaride hilo. Kabla ya kukagua gwaride lenye umbo la Alfa mizinga mingine 21 na baada ya hapo ndipo alipoenda kukagua gwaride hilo huku ndege vita zikipita angani.

 Rais Magufuli baada ya kumaliza kukagua gwaride alienda moja kwa moja jukwaa kuu.Wakati huo wananchi na wageni waalikwa wote walikuwa wamesimama huku shangwe zikiwa zimetawala.Gwaride liliendelea kutoa burudani na kisha kufuatiwa tena na wimbo wa Taifa.

Hata hivyo gwaride maalum ambalo liligawanyika katika sehemu tatu ikiwemo waliobeba bendera ya Rais.Gwaride hilo lilipita mbele ya Rais Magufuli.Katika sherehe hizo burudani za kila aina zimetawala.Hata hivyo gwaride likipita mbele ya Rais shangwe zilitawala uwanjani hapo.Shangwe ilikuwa zaidi walipoingia makomandoo.

Baada ya gwaride kutoka uwanjani ilifuata hatua ya utambulisho wa wageni waliohudhuria tukio hilo la kihistoria ambalo hutokea kila baada ya miaka mitano.Baadhi ya wageni hao ni Rais wa Uganda, Yoweri Museven, Rais wa Comorro Kazar Othaman na  Rais wa Zimbabwe Emmason Mnangagwa.Pia wametambulishwa wawakilishi wa nchi mbalimbali pamoja na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania.


No comments: