LHRC YAENDESHA MAFUNZO YA SHERIA ZA UHURU WA HABARI KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA
Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa mafunzo ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre - LHRC) kimetoa mafunzo ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa ili kuwajengea uwezo kuzielewa sheria zinazoongoza Tasnia ya Habari nchini.
Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameanza leo Jumapili Novemba 15,2020 Mjini Shinyanga yamekutanisha pamoja waandishi wa habari 23 kutoka mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Mara.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale amesema mafunzo hayo yatawawezesha waandishi wa habari kuzijua sheria zinazohusu tasnia ya habari ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri.
“Mafunzo haya yanahusu haki za binadamu, Uhuru wa Kushiriki 'Civic Space' ambapo tunawajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sheria mbalimbali zinazogusa Tasnia ya Habari kama vile Kanuni za Mawasiliano ya Kielekroniki na Posta 'Maudhui ya Habari Mtandaoni) 2020, Sheria ya makosa ya mtandao 2015, Sheria ya Huduma ya Habari 2016 na Sheria ya kupata habari 2016",amesema Ntwale.
Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sheria hizo ili waweze kufanya kazi katika mazingira salama na kwa kujiamini ili kupunguza kesi zinazowakumba waandishi wa habari zinazotokana na kukiuka sheria bila kujua.
"LHRC inaendesha mafunzo juu ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa waandishi wa habari nchini Tanzania katika Kanda saba na kwa Sasa imefikia Kanda ya Ziwa ambapo tumeamua yafanyike mkoani Shinyanga",ameongeza Ntwale.
Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa mafunzo ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa leo Jumapili Novemba 15,2020 katika Ukumbi wa Shinyanga Fairies Hotel Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa mafunzo ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa.
Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa mafunzo ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa.
Wakili wa Kujitegemea Pasience Mlowe akitoa mada kuhusu Uhuru wa Kujieleza wakati wa mafunzo kuhusu sheria za Uhuru wa Habari yaliyoandaliwa na LHRC.
Wakili wa Kujitegemea Pasience Mlowe akitoa mada kuhusu Uhuru wa Kujieleza wakati wa mafunzo kuhusu sheria za Uhuru wa Habari yaliyoandaliwa na LHRC.
Washiriki wakiwa ukumbini
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Waandishi wa habari/washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Mafunzo yanaendelea
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments: