KIMEI KUTUMIA UZOEFU WAKE WA MIAKA 21 WA KIBENKI KULINYANYUA JIMBO LA VUNJO
MBUNGE wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, Charles Kimei amesema atatumia uzoefu wake aliokua nao wa miaka 21 wa kuongoza moja kati ya Taasisi kubwa za Kibenki nchini katika kuwatumikia wananchi wa Jimbo lake.
Akizungumza na Michuzi Blog mara baada ya kuapishwa leo kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano ww Tanzania, Kimei amesema atatumia uzoefu wake katika kushirikiana na watendaji wa serikali pamoja na wananchi ili asiwepo mwananchi anaelalamikia viongozi na badala yake wanufaike na viongozi waliowachagua.
" Ninaporudi sasa kule jimboni baada ya kuapa basi tunaenda kutekeleza yale yote niliyoyaahidi Ikiwa ni pamoja na kuhamasisha watu ili kwa pamoja tueze kushirikiana kuinyanyua Vunjo yetu na wala asiwepo kijana anayekaa kijiweni bali wote wajikite katika miradi mbalimbali ambayo tutashirikiana nao kuianzisha. Kwa upande wa miundombiniu tutashirikiana na serikali kwa ukaribu sana pale tutakapolazimika ambapo tutakua tunahitaji rasilimali kubwa pale inapohitajika ndogo tutachangia hivyo. " Amesema Kimei.
Amesema ana bahati kubwa ya kuitumikia Taasisi kubwa ya Kibenki kwa miaka 21 hivyo anao uwezo mkubwa wa kuwawezesha wananchi wetu kujiinua kiuchumi na kijamii, kuwahamasisha vijana kuepuka kukaa vijiweni na kuwatafutia miradi ili waweze kujiajiri.
Mbunge huyo pia amewashukuru wananchi wa Jimbo hilo kumchagua kwa kura za wingi na kishindo kwa asilimia zaidi ya 80 Dk John Magufuli kuwa Rais kwa kipindi kingine na yeye kumchagua kwa asilimia 72 kuwatumikia wananchi wa Vunjo.
No comments: