KAMATI YA MADINI YA TANZANITE/MAREMA WAMPONGEZA DKT.MAGUFULI.
Mwenyekiti wa (MAREMA)ndugu Jastin Nyari akizungumza na waaandishi was habari leo Ofisini kwake Jijini Arusha Makamu Mwenyekiti wa Madini ya Tanzanite Tanzania Nene John Lyimo
Wa Kwanza kushoto ni Makamu wenyekiti wa Madini ya Tanzanite Tanzania Nene John Lyimo,akiwa na Naibu katibu wa MAREMA mkoa wa Manyara Joseph Bahati
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Kamati ya madini ya Tanzanite Tanzania iliyopo chini ya Shirikisho la wachimbaji madini Tanzania( FEMATA )kwa kushirikiana na Chama Cha wachimbaji wa madini mkoa wa Manyara (MAREMA) imetoa pongezi kwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwa awamu nyingine kwa kishindo.
Akizungumza na waaandishi was habari ofisini kwake Mwenyekiti wa (MAREMA)
Jastin Nyari amesema kuwa kazi alizozifanya Dkt.Magufuli katika awamu iliyopita ndiyo imepelekea yeye kuchaguliwa tena .
Nyari amesema kuwa miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na ujenzi wa ukuta Mererani,ambapo umesababisha dunia kutambua kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee yanapopatikqna madini Tanzanite,tofauti na ulaghai was nchi zilizokuwa zinajipatia ujiko
Sambamba na hayo ufutaji wa Kodi kwa wachimbaji wadogo uliopelekea kupatikana kwa wingi wa madini,Ujenzi wa masoko ya madini ,ambapo mchimbaji akipata madini makubwa Serikali inayanunu tofauti na awali walikuwa hawajui watayauzia wapi
Nyari amesema kuwa kumekuwa na changamoto za vifaa vya kuchimbia madini ,ikiwepo milipuko,ambapo imekuwa ikifika nchini na kupelekwa kwa wachimbaji wadogo wadogo kwa bei ya juu, amemuomba Rais kupitia wasaidizi wake Wizara ya madini na TRA, waangalie uwezekano wa kupunguza gharama ya Kodi, ili wachimbaji waweze kununua vifaa hivyo kwa bei rahisi.
Kwa niamba ya wachimbaji madini Nyari ameiomba Wizara husika iangalie uwezekano wa kutoa kibali , ili Kama wanakosa upande katika kampuni ,kibali kile kimuwezeshe mchimbaji kwenda kununua kwenye kampuni nyingine
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Madini ya Tanzanite Tanzania Nene John Lyimo ,amesema kuwa wanayo matumaini makubwa kwa kuchaguliwa tena kwa Dkt.Magufuli ,wameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza wigo wa walipa Kodi ,kwaajili ya kuongeza pato la Taifa
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kutambua kwamba uchaguzi umemalizika ,kilichobakia ni kuongeza bidii katika utendaji, wasibweteke ,waelekeze nguvu zao zaidi katika utendaji kazi kwa manufaa yao,kwa jamii na Taifa kwa kuujenga Uchumi wa Kati, na wa juu zaidi.
No comments: