DKT. STEPHAN NGAILO AWAONDOA WASIWASI WAKULIMA WA MKOA WA MBEYA

../Downloads/IMG-20201123-WA0088.jpgMkurugenzi Mtendaji waMamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt Stephan Ngailo akipewa maelezo kutoka kwa Afisa wa Kampuni la Eka Moja Ltd linalotoa mikopo ya mbolea kwa wakulima katika Halmashauri ya Wilaya  ya Mbozi. 

../Downloads/IMG-20201123-WA0087.jpg

Wafanyakazi wa moja ya maghala ya mbolea mkoani Songwe  wakishusha mbolea  kwenye  gari na kuhifadhi katika ghala hilo tayari kwa kuwauzua wakulima   wakati  huu wa msimu wa kilimo.

/Users/sixmund/Downloads/IMG-20201120-WA0086.jpg

Pichani ni sehemu ya shehena ya Mbolea iliyohifadhiwa kwenye moja ya maghala Mkoani Mbeya


Na Mwandishi wetu

Wakulima Mkoani Mbeya watakiwa kuondoa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa Mbolea Mkoani humo na kuwa waendele na maandalizi ya mashamba yao ili kwendana na msimu huu wa kilimo nchini.


Hayo yamesemwa na Mtendaji  wa Mamlaka  ya Mbolea  Tanzania  Dkt. Stephan Ngailo katika ziara yake kwa lengo lakujionea hali ya upatikanaji na usambaziji wa Mbolea nchini ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya wakulima kwenye Mikoa yote inayo jishughulisha na kilomo cha mazao mbali mbali ya chakula na biasha.


Dkt Ngailo amesema kuwa ameridhishwa na uwepo wa mbolea ya kutosha kwenye Maghala mbali mbali yaliyopo Mkoani Mbeya, huku akiwapongeza wafanyabiashara ya bidhaa hiyo kwa kufuata sherili na taratibu zote zilizowekwa na Serikali pamoja na kutoa mikopo ya mbolea kwa zaidi ya wakulima 25000 pia amekerwa na wafanya biashara wachache wanaokiuka taratibu zilizopo.


Nimefika Mbalizi, Chunya na hapa Mbeya, nimerithishwa sana na uwepo wa mbolea ya kutosha, pia nimeridhishwa sana na uwadilifu wa wawanyabiashara ya Mbolea hapa Mbeya wanafanya kazi nzuri sana, ila nimekerwa sana na wafanya biashara wachahe, wanao kiuka utaratibu kwa kufungua mifuko ya mbolea na kuuza kwa kupima, hawa tutawashughulikia” Alisema Dkt Ngailo


Ili kuongeza tija kwenye kilimo, Dkt Ngailo amewashauri wakulima kuzingatia kanuni za kilimo bora ambacho ni pamoja na kuchagua eneo sahihi, kupanda kwa wakati, kupanda mbegu kwa usahihi pamoja na kuweka mbolea kwa husahihi na wakati sahihi.


Mkurugenzi Mtendaji  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo anaendelea na ziara yake ya kukagua na kujionea hali ya upatikanaji na usambaziji wa Mbolea nchini kwenye Mikoa ya Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma na Tabora.

No comments: