DKT MAGUFULI AAHIDI KUMALIZIA MIRADI YA MAJI ILIYOSALIA. MIRADI 1,422 IMEKAMILIKA

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema ndani ya miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano wameweza kutekeleza jumla ya miradi ya maji 1,422 yenye thamani ya Sh trillion 2.2.

Akihutubia wakati wa uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jijini Dodoma, Magufuli amesema serikali ya awamu ya tano wamefanikiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa maeneo ya vijijini toka asilimia 47 mwaka 2015 hadi asilimia 60.1 mwaka 2020.

Akielezea upatikanaji wa maji kwa mijini, Magufuli amesema “Kwa maeneo ya mijini, tumefanikiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi asilimia 84 kwa mwaka 2020,”

Aidha, amesema serikali yake itasimamia utekelezaji wa miradi wa kutoa maji Ziwa Victoria unaogharimu Sh billion 600 na mradi mkubwa wa maji wa Arusha kwa gharama ya Sh billion 520 ili wananchi wa maeneo hayo wapate majis afi na salama na kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.

“Kwa miaka mitano ijayo, serikali itahakikisha mito na maziwa yetu inatumika kikamilifu katika kuwafikishia maji wananchi wa maeneo husika,” Magufuli.

Mbali na hilo katika kipindi cha miaka mitano, Mamlaka mbalimbali zimeweza kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji ikiwemo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dar Es Salaam (DAWASA) chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja wameweza kusimamia miradi ya maji mikubwa kwa kutumia fedha za ndani ikiwemo mradi wa Kibamba Kisarawe uliogharimu Bilioni 10.6 unaohudumia Mkoa wa Kihuduma Kisarawe.

Pia, Dawasa wameweza kuongeza mapato yao ndani baada ya kudhibiti kwa kiasi kikubwa mivujo (mabomba yaliyopasuka) na wateja wapya kuunganishwa kutokana na upatikanaji mzuri wa huduma ya maji hususani katika maeneo yaliyokuwa na changamoto ya huduma hiyo kwa muda mrefu.

Katika mikakati ya Mamlaka hiyo ndani ya miaka mitano kuanzia 2020/25 ni kuhakikisha maeneo yote ambayo mtandao wa Dawasa haujafika basi wanafika kwa asilimia kubwa na kuondoa kero ya maji ya wananchi.


 

No comments: