CHUO CHA KODI KUJENGA TAWI JINGINE KIBAHA PWANI, MAHAFALI YA 13 YAFANA

Kamisha wa fedha na manunuzi  wa Wizara ya Fedha na Mipango, Fredrick Mwakibinga akizungumza katika mahafali ya 13 ya chuo cha Kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamisha wa fedha na manunuzi  wa Wizara ya Fedha na Mipango, Fredrick Mwakibinga akitoa vyeti na zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo.

 KATIKA  kuongeza tija katika utoaji elimu hapa nchini Chuo Cha Kodi kimeomba Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa Chuo hicho katika eneo lililopo Kibaha Mkoani Pwani.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo Cha Kodi, Profesa Isaya Jairo wakati akizungumza katika mahafali ya 13 ya chuo cha kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salam leo Novemba 27,2020. Amesema kuwa michoro ya ramani za majengo zimeshakamilika na bajeti tu ndio inasubiriwa ili ujenzi uanze.

Hata hivyo katika mahafali hiyo  wahadhiri waliofanya tafiti mbalimbali katika kipindi cha masomo cha 2019/2020 na tafiti zao kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya kitaaluma na katika jarida la Chuo cha Kodi metunukiwa vyeti.

Na wahitimu wa ngazi mbalimbali za masomo waliofanya vizuri wamepewa zawadi mbalimbali na fedha.

 Hata hivyo kwa mwaka wa masomo wa 2019/2020 wahitimu 384 wametunukiwa ngazi ya Cheti, Stashada na Shahada na Stashahada ya Uzamili.

Jumla ya Wahitimu  160 wametunukiwa cheti Cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki (CFFPC) ikiwa na wanawake 103 na wanaume 57.

Kwa Upande wa Cheti cha Awali Cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM) wahitimu 18 wametunukiwa ikiwa Wanawake 5 na wanaume 13.

71 wametunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (DCTM) wanawake 33 na wanaume 38 huku Jumla ya watunukiwa wa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) 117 ikiwa wanawake 58 na wanaume 59.

Hata hivyo watunukiwa wa Stashahada ya Uzamili katika Kodi wakiwa 18 wanawake wakiwa 4 na wanaume 14 wakifanya jumla ya watunukiwa wote kuwa 384.

Kwa Upande kwe Mgeni Rasmi ambaye alimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango, Kamishna wa Fedha na Manunuzi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Fredrick Mwakibinga amesema kuwa maombi yao yatafanyiwa kazi kwani yote ni malengo mazuri katika kuendeleza ubora wa elimu hapa nchini.

Hata hivyo amewapongeza wahitimu wote na kuwasihi wajingine na maradhi mbalimbali hasa Ukimwi.

No comments: