CAMFED YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA SINGIDA
Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Yasinta Alute akifungua mafunzo ya elimu ya utambuzi juu ya mambo mbalimbali kwa wasichana yanayofadhiliwa na CAMFED, ikiwemo uelewa ya afya ya uzazi, UKIMWI, Ujasiriamali na namna ya kubaini fursa zinazozunguka jamii na njia bora ya kuzifikia mkoani Singida jana. Kulia ni Mjumbe wa shirika hilo Paschal Kichambati, Mkuu wa Miradi Nasikiwa Mwalisu na Mwenyekiti wa CDC Manispaa ya Singida, Omary Kisuda.
- Mkuu wa Miradi Nasikiwa Mwalisu akitoa mada kwenye mafunzo hayo.Mwenyekiti wa CDC Manispaa ya Singida, Omary Kisuda akizungumza.
Washiriki kutoka Wilaya za Manyoni na Singida Manispaa wakifuatilia mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mwenyekiti wa CAMA wilaya ya Manyoni, Bahati Ismaili akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.Mafunzo yakiendelea.
Na Godwin Myovela, Singida
SHIRIKA lisilo la kiserikali la CAMFED limewataka wasichana mkoani hapa kutobweteka, na badala yake kutazama fursa zinazowazunguka na kuzigeuza kuwa chanzo cha kuinua kipato katika muktadha chanya wa kuibadili jamii kimaendeleo.
Imeelezwa stratejia mojawapo itakayowasaidia wasichana hususani wale waliojifungua katika umri mdogo -ni kuwawezesha kwa kuwajengea pamoja na mambo mengine, misingi ya kutambua haki ya wao kupata elimu juu ya afya ya uzazi na UKIMWI.
Akizungumza mkoani hapa wakati wa mafunzo hayo ya kuwawezesha kujitambua, sambamba na kutambua fursa mbalimbali zinazowazunguka nje ya mfumo rasmi wa elimu, Mkuu wa Miradi kutoka Camfed, Nasikiwa Mwalisu alisema kama mtoto wa kike akijilinda na kuwa na utambuzi wa magonjwa basi atakuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa na kutimiza ndoto zake za maisha.
“Kundi hili kama lisipoangaliwa kwa makini na kupewa elimu hii ya utambuzi juu ya mambo mbalimbali, ikiwemo elimu ya uzazi na kujikinga na magonjwa linaweza kupoteza mwelekeo, ambao madhara yake huwa ni makubwa...lakini pia athari zake husambaa kwa jamii na taifa kwa ujumla,” alisema Mwalisu.
Aidha, kuhusu sera ya ulinzi na usalama wa mtoto, Mwalisu alisema jamii inapaswa kutambua na kuheshimu takwa hilo la msingi la mtoto kupata elimu, kuheshimiwa, kupendwa na kulindwa kama haki ya msingi na sio hiari, lengo hasa ni kujenga ustawi na taswira chanya ya ukuaji wake kisaikolojia na kiafya.
Kwa upande wake, Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Yasinta Alute alisema afya njema ni matokeo ya kila kitu katika maisha na ustawi wa ukuaji wa mtoto. Alisisitiza kama rika hilo la mtoto wa kile likipatiwa mafunzo ya mara kwa mara juu ya utambuzi kwenye nyanja mbalimbali- mfano wa hayo yanayowezeshwa na ‘Camfed’ ni dhahiri litageuka chachu katika kuleta maendeleo kwenye jamii.
“Ukipata mafunzo ya afya ya uzazi na ukajitambua huwezi kukosea wala kurudia tena makosa…nawaomba ninyi mliobahatika kupata mafunzo hayo mkawe chachu na mabalozi kwa wengine,” alisema Alute huku akiwaomba Camfed Makao Makuu kuangalia namna ya kupanua wigo wa huduma zao kwenye wilaya nyingine mkoani hapa ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika.
Awali, Afisa Elimu Sekondari na Mwenyekiti wa Kamati ya Wilaya ya Camfed Manispaa ya Singida, Omary Kisuda, alisema jumla ya wasichana 60 kutoka Singida Manispaa na wilaya ya Manyoni wanaendelea kupewa mafunzo kupitia programu ya elimu ya utambuzi kwa mtoto wa kike yaani ‘Tanzania Campaign for Female Education’
“Hili ni rika la wao kujiendeleza kielimu, biashara, ujasiriamali, na elimu ya afya ya uzazi na ndio sababu hasa ya kuwakutanisha na kuwapa mafunzo haya muhimu ya utambuzi chini ya ufadhili wa Camfed na Serikali,” alisema Kisuda.
No comments: