BODI YA FILAMU YAJIONEA UANDAAJI WA TAMTHILIA YA SHILINGI
Bodi ya Filamu Tanzania imeendelea na utaratibu wa kuwatembelea wadau wa Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza katika mandhari ya kazi zao ili kuona, kujifunza, na kujadili kwa pamoja namna ya kukuza Tasnia hiyo.
Tarehe 09 Novemba, 2020 Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo, Dkt. Kiagho Kilonzo alizuru eneo ambalo watendaji (film crew) wa An Omary Production walikuwa wakiandaa Tamthilia ya Shilingi.
Pamoja na kuona uandaaji wa Tamthilia hiyo, Dkt. Kilonzo aliwaelezea mikakati ya Bodi katika kukuza Sekta ya Filamu kupitia mafunzo, ambapo alieleza uwepo wa mafunzo maalum yanayotolewa kwa njia ya uchambuzi wa Filamu (Screening/Criticism) ambayo yanadhaminiwa na Goethe Institut. Vilevile, alieleza hivi karibu kutakuwepo na mafunzo kwa vitendo katika maeneo ya Uhariri, Uongozaji, Upigaji Picha na Uigizaji.
Zoezi la kuwatembelea wadau katika mandhari zao za kazi limekuwa kilifanyika mara kwa mara ambapo Bodi imeshatembelea Wazalishaji mbalimbali wakiwemo wa Tamthilia ya Huba, Kapuni, na Slay queen.
No comments: