WIZARA YA MAJI YASAINI MAKUBALIANO YA UTENDAJI BAINA YAKE NA BODI ZA MAJI ZA MABONDE
Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imewaagiza maafisa maji wa bodi za maji na mabonde kusimamia kikamilifu rasilimali za maji, kudhibiti uchafuzi na kuhakikisha matumizi sahihi ya maji kwa ajili ya maendeleo ya jamii yanakua bora.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya utendaji kazi wa bodi za maji za mabonde kwa mwaka 2020 ambapo amesisitiza kuwa sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji imezipatia bodi za maji za mabonde jukumu la kusimamia rasilimali za maji na Wizara imekua ikiwezesha kifedha ili kutekeleza miradi pamoja na majukumu ya usimamizi wa rasilimali za maji.
Mhandisi Sanga amesema lengo la kusaini makubaliano ya utendaji ni kuweka viashiria vya kupima utekelezaji sa malengo ambayo bodi za maji za mabonde zimejiwekea na kuwezesha wizara kufanya tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa kazi za bodi za maji na mabonde.
" Nimetaarifiwa kwamba tathmini ya utekelezaji wa makubaliano kwa mwaka 2019/20 imefanyikia ikihusisha bodi za maji za mabonde yote tisa nchini, zoezi la tathmini limefanyika kwa njia ya usajili, ukaguzi wa taarifa na kutembelea maeneo yaliyofanyiwa kazi.
Matokeo ya tathmini iliyofanyika yameonesha kuwa utendaji wa bodi zote kwa mwaka 2019/20 ulikua ni wastani wa asilimia 56.2 kwa sehemu kubwa bodi zilifanya vizuri kwenye maeneo ya Water Resources Governance kwa asilimia 58," Amesema Sanga.
Amesema mambo yalichangia kuwa na wastani mzuri wa utekelezaji katika maeneo hayo ni pamoja na uanzishwaji wa Jumuiya za watumiaji maji na kufanyika kwa vikao kazi vya mara kwa mara.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akitia saini makubaliano ya utendaji baina ya Wizara na Bodi za Maji za Mabonde leo jijini Dodoma.
Maafisa ja Wenyeviti wa Bodi za Maji na Mabonde wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga leo jijini Dodoma.
No comments: