Wana Msambweni mlijua kutukirimu kwa kila bashasha ,Tunatumai nyinyi na wana Tanga kwaujumla mtajitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 28,2020 - UMMY
Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuwa mwakilishi wa wana Tanga atahakikisha fedha za Tasaf zinawanufaisha walengwa na si wengine kama ilivyo sasa.
Mgombea Ubunge ,Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano wa kuinadi Ilani ya Ccm na kuomba ridhaa ya Wananchi kuwa Mbunge Amesema “Ndugu zangu wanamsambweni nafahamu kero mojawapo inayowasumbua nyinyi na wana Tanga kwaujumla ni fedha za Tasaf kutowafikia walengwa,na hali hii inasabishwa na baadhi ya watendaji wetu wasio waaminifu,ambao huwapatia fedha watu wasiostahili kupewa Niwaambie jambo hili nimeanza kulifanyia kazi tutahakikisha wakazi wa Msambweni na Tanga nzima wanaostahili kupata fedha za Tasaf wanapata”Amesema Ummy Mwalimu.
Aidha Ummy ameahidi pia kutatua changamoto ya Elimu kwakusukuma maboresho ya Miundombinu katika Shule ya Msingi Msambweni na Sekondari yake,Daraja kutoka Chuo cha Zaharau hadi Ofisi ya Kata ,na kusafisha dimbwi la Maji linalozalisha mbu katika Mtaa wa Msambweni C .
No comments: