Teknolojia ya digitali ilivyo msingi wa uchumi imara siku zijazo
Mandara Mdava, UDSM
Habari hii pamoja na habari ya juma hili ya makadirio ya ukuaji wa uchumi inadhihirisha kuwa nchi imefkia hatua madhubuti katika muelekeo wake wa maendeleo. Hivyo, ni muhimu sasa tukaendelea kushikilia mwendo huo huo ili kuhakikisha kuwa manufaa yake yanawafikiwa watu wote nchini.
Kumekuwepo na mjadala miongoni mwa wanazuoni barani Afrika juu ya namna nchi za Afrka zinaweza kuendelea kuhakikisha ukuaji wa uchumi wake.
Uchunguzi wa hivi karibuni wa Harvard Business Reviews umeeleza namna teknolojia ya kidijitali, ikiwa ni pamoja na intaneti kwenye simu, programu tumishi (App) na simu za mkononi, vimekuwa vichocheo vikubwa kufanikisha lengo hili. Uchunguzi huo umeeleza kuwa huduma hizo zinata fursa za kiuchumi na kuwezesha mfumo wa kifedha jumushi.
Ni muhimu kukumbuka mchango mkubwa wa kampuni za mawasiliano ya simu katika kufanikisha hilo. Kwa miaka mingi sasa kmapuni hizi zimekuwa na mchango mkubwa katika kutoa huduma za kuboresha maisha ya wanajamii ambazo zimekuwa zikifurahiwa na wateja wote.
Mbali na hilo, kampuni kama Tigo Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inaondoa utofauti (gap) wa upatikanaji na matumizi ya teknolojia kati ya maeneo ya mjini na vijijini. Tigo imewawezesha hata wale wanaoshi maeneo ya vijijini kupata huduma bora kwa njia ya simu kama vile Tigo Pesa.
Aidha, Tigo pamoja na washindani wengine wamehusika katika kutoa ajira kwa maelfu ya kwenye vitengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafundi, mawakala wa huduma za fedha pamoja na wote wanaofanyakazi kwenye stoo. Kwa ujumla, si jambo la kushangaza kuwa GSMA imekadiriwa kuwa sekta ya mawasiliano ya simu ndio inatoa mchango mkubwa zaidi kwenye uchumi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Katika ripoti ya hivi karibuni kwa mfano, imeeleza kuwa kwa mwaka 2019, sekta hiyo ilichangia USD bilioni 155.
Wakati nchi ikiwa imeingia katika ukurasa mpya kwenye safari yake kuelekea mapinduzi ya kiuchumi, tuangazie ni kwa njia gani ambazo kampuni hizi za simu zinaweza kuendelea kutoka mchango wa kiuchumi.
Kwa kujidhatiti na kuwekeza kwenye miundombinu na huduma, kampuni za mwasiliano zitaweza kuhakikisha kuwa watu zaidi wananufaika na huduma bora za kimapinduzi ambazo teknolojia ya simu itaendelea kuzileta katika miaka ijayo.
No comments: