SGA yatoa vifaa vya michezo shuleni


KAMPUNI ya ulinzi ya SGA imetoa vifaa vya michezo katika shule za msingi hapa nchini, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya Wiki ya Huduma kwa Wateja (Customer Service Week) ambayo ilifikia tamati mwishoni mwa wiki.

Lengo la kuchangia vifaa hivyo ilikuwa kurudisha wema katika jamii, kwa kuwapa nguvu wanafunzi kipindi cha masomo yao.

Maofisa wa kampuni hiyo walihudhuria matukio mbalimbali ya ugawaji wa vifaa hivyo na sherehe za kuwaaga wanafunzi wa darasa saba, ambao wamemaliza elimu ya msingi.

Baadahi ya shule za msingi zilizofaidika na vifaa hivyo vya michezo ni Mirambo iliyopo Lugalo, ambapo katika tukio la ugawaji, wanafunzi zaidi ya 150 walihitimu elimu ya msingi ya darasa la saba.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo  alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,  Eric Sambu, mgawaji wa vifaa hivyo pamoja na bidhaa nyingine ambazo zitawasaidia wanafunzi, kujifunza wakiwa shuleni.

Alitoa mifano ya watu maarufu kama vile Mbwana Samatta and Diamond Platinumz ambao wamefanya bidii na kufuata ndoto zao na wamepata mafanikio makubwa huku akiwaambia wanafunzi kuwa na wao wanaweza kufanikiwa wakidhamiria na kuwa na ndoto maishani.

Mkuu wa shule hiyo, Bi Rehema Matomoki aliishukuru SGA security kwa msaada huo na kutoa rai kwa mashirika mengine kuiga mfano huo. Alisema licha ya mazingira magumu shule hiyo imejitahidikupata mafanikio na wataendelea kufanya bidii ili wapate matokeozaidi.

Shule nyingine iliyofaidika ni Shule ya msingi ya Arusha,  iliyowakilishwa na  Victor Gaudence ambaye aliwahi kusoma pale.

Victor alitoa changamoto kwa wanafunzi hao wamuige yeye na wengine waliosoma shuleni hapo na sasa ni watu maarufu. Alisema sule hiyo ina historia kubwa mno kwani ilianzishwa tangu enzi za ukoloni huku aitoa wito kwa wanafunziwa zamani wakumbuke kurudi kutoa misaada mbalimbali katika shule hiyo ili iendelee kufanya vizuri.

Katika hatua nyingine, Sambu alisema, SGA ina lengo la kuisaidia jamii, na usalama katika maeneo mbalimbali.

“SGA ni kampuni binafsi, tukidhihirisha hilo kwa kazi zetu, ambazo tumefanya kwa bidii, tuna wafanyakazi 18,000 katika kampuni kote duniani katika kampuni  iliyoanzishwa miaka ya 50 iliyopita na wamepitia mafunzo mengi kwa ufanisi” alisema Sambu.

Alisema kampuni hiyo imeweza kuendeleza ubora tangu 2001 ilipotambuliwa kupitia cheti cha ISO certification na hivi karibuni wametambuliwa na OSHA  kupitia ISO 45001. Pia ni kampuni ya kwanza ya ulinzi Tanzania kupokea cheti cha ISO 18788 kwenye masuala ya usalama.

SGA ndio kampuni kongwe binafsi ya ulinzi Tanzania ambayo ilianzishwa mwaka 1984 huku ikijulikana kama Group Four security na kwa sasa imeajirizaidi ya wanfanyakazi 5,800 nchi nzima.

Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security, Eric Sambu (kulia) akikabidhi vifaa vya michezo kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mirambo ya Jijini Dar es Salaam, Rehema Matomoki huku mmoja wa  walimu wa shule hiyo wakishuhudia. Msaada huu ulikuwa sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja (Customer Service Week) ambapo baadhi ya shule nchini zilifaidika na masaada huo.

No comments: