SERIKALI YATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE KWA MAKUNDI MAALUM


Dc wa monduli Edward Balele,Mkurugenzi wa shirika la okoa new generation,wakimkabidhi tuzo mwenyekiti wa shivyawata albino katika eneo la mto wa mbu wilayani Monduli mkoa Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele akisalimiana na mmojawa mmoja wa Washiriki mwenye ulemavu Kama inavyoonekana katika picha

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele,Mkurugenzi wa Shirika la Okoa New Generation Bi Neema Mgendi wakati wa Tamasha la kutambua shughuli zinazofanywa na vikundi vya watu hao na vikundi vya Vijana Mto wa Mbu.

Mkurugenzi wa Shirika la Okoa New Generation Bi Neema Mgendi,akisalimiana na ndugu William Saning'o wakati wa Tamasha la kutambua shughuli zinazofanywa na vikundi vya watu hao na vikundi vya Vijana Mto wa Mbu.



===== ====== = ====== =====



Na.Vero Ignatus,Monduli.


Serikali imetakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuendelea kutoa kipaumbele kwa kuwasaidia watu wa makundi maalumu yenye uhitaji ili kupunguza Utegemezi katika jamii na kuweza kufikia malengo yao kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt,JOHN MAGUFULI.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika la Okoa New Generation Bi Neema Mgendi wakati wa Tamasha la kutambua shughuli zinazofanywa na vikundi vya watu hao na vikundi vya Vijana Mto wa Mbu; vinavyosimamiwa na Shirika la Okoa New Generation kwa ushirikiano na serikali lililofanyika katika kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli Mkoani Arusha.

Hata hivyo amesema kuwa endapo suala hili la kutoa kipaumbelle linahitaji kila moja ashiriki ili kuwezesha kundi hilo kwa kuliondolea changamoto mbalimbali ambazo wanazo.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele ambae alikuwa mgeni rasmi pia amesema kuwa Serikali inaunga mkono jitihada zinazofanya na makundi maalum na ameahidi kutatua changamoto zinazokabili shirika hilo.

Pia amelishukuru shirika la Okoa New Generation kwa kuwasaidia watu wa makundi maalum yenye uhitaji huku akiahidi kusimamia ombi la watu hao kupata eneo kwa ajili ya kuuza bidhaa zao pamoja na kuwatafutia soko la uhakika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa SHIVYAWATA wilayani Monduli Bi. Dorah Msuya ambalo ni Shirikisho la vyama vya watu wa makundi maalumu yenye uhitaji Tanzania SHIVYAWATA Pamoja na vikundi mbalimbali ya watu hao wilayani Monduli mkoani Arusha wameishukuru serikali kwa kukumbuka kundi hilo ambalo linahitaji kupewa kipaumbele na kuwaondoa katika lindi la umasikini kwa kuruhusu kupewa mikopo isiyo na riba.

Mwenyekiti Bi. Dorah Msuya pamoja na Mwenyekiti wa Kikundi cha Nuru Disaibod Bwana Khalfan Sabuni wamesema kwa sasa wana miradi wanayoifanya ambayo imewapatia mikopo ambapo wanaweza kuhudumia familia zao pamoja na kujipatia mahitaji muhimu ya kibinaadamu.

Licha ya jitihada wanazozifanya kujikwamua kiuchumi lakini mafanikio hayo bado kundi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo sehemu ya kufanyika kazi zao ambapo wameiomba Serikali Wilayani Monduli iwasaidie kupata eneo hilo ili waweze kufanya kazi zao bila kubugudhiwa.

Aidha Afisa Uendelezaji wa Biashara kutoka Sido mkoani Arusha Bi .Bahati Mkopi amesema Sido wanashirikiana na Okoa New Generation katika kuwawezesha wajasirimali wabunifu hasa watu wa makundi maalumu kwa kuwajengea uwezo katika masuala ya ubunifu na teknolojia.

Kwa upande wao wanachama wa shivyawata wamesema kuwa mikopo waliyopewa imekuwa msaada mkubwa kwao kubadili maisha yao ya kila siku na kukuza uchumi kwa familia na jamii kwa ujumla.

Katika maonesho hayo watu hao walionesha bidhaa mbalimbali wanazozalisha kupitia mikopo waliyopewa na halmashauri ikiwemo za kilimo, mifugo, bidhaa za sabuni, shanga, pamoja na bidhaa zitokanazo na vitenge.

No comments: